Waziri wa maji ,Jumaa Aweso akizungumzia mafanikio ya sekta ya maji katika mwaka mmoja wa serikali awamu ya sita Jijini Arusha (Happy Lazaro)
*****************
Happy Lazaro,Arusha
Arusha .Serikali imejipanga kupunguza changamoto hali ya ukosefu wa maji katika jiji la Dar es Salaam kwa kuanzisha mradi wa ujenzi wa bwawa la kidunda ili mitambo ya Ruvu chini na juu kuweza kusaidia upatikanaji wa rasilimali hiyo
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Arusha,Waziri wa maji Jumaa Aweso amesema jiji hilo limepata changamoto ya upungufu wa maji safi na salama kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa nakupelekea kina cha maji cha mto Ruvu chini na juu kupungua.
“Kutokana na changamoto ya kupungua kwa kina cha maji katika Mto Ruvu chini na juu hali iliyosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa serikali imekuja na mkakati wa uchimbaji bwawa ya kuvuna maji ya mvua ili wananchi Dar es salaam waweze kupata huduma safi na salama,”amesema Waziri.
Aweso amesema kutokana na upotevu wa maji ya mvua kupotea hivyo ujenzi wa bwawa la kidunda utakusanya maji kwa lengo la kusaidia wananchi katika shughuli zao hasa katika kilimo cha umwagiliaji.
Aidha amesema hatua waliofikia katika ujenzi wa bwawa hilo ni kutangaza zabuni katika mradi huo wa kidunda ambao utakwenda kupunguza changamoto ya maji katika jiji hilo na mkoa wa Pwani kupitia mradi wa mto rufiji.
Waziri huyo amesema kwa upande wa jiji la Arusha mahitaji yake ya maji ni lita milioni 109 ambapo mradi wa sh.bilioni 520 wenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 200 hivyo ukikamilika maeneo yote ya mkoa huo yatapata maji.