***********************
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
March 6
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, ambae pia ni Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, ameingilia kati mgogoro wa kwenye Hifadhi ya Uzigua Kijiji cha Kwamduma kata ya Kibindu na kuutatua .
Hayo yamejiri kwenye muendelezo wa ziara ya mbunge huyo ambapo alitembelea Vijiji vilivyopo kata ya Kibindu.
Mkazi wa Kwamduma Hussein Shafii amemshukuru Mbunge na Naibu Waziri kwa kutatua mgogoro huo.
Nae Selemani Hamis akapongeza jitihada zake za kusukuma ukarabati wa barabara kila mara ikiharibika huku sasa hivi ikijengwa barabara kubwa kutoka kwa Luhombe mpaka Gole ambayo Mkandarasi yuko barabarani anajenga barabara hiyo .
Pia Wananchi wa Kata hiyo wamemshukuru Rais Samia kufanikisha kujenga Kituo cha Afya Kibindu ambapo Rais Samia alipeleka fedha pamoja na ununuzi wa gari ya kubebea wagonjwa ‘Ambulance’, na usimamizi wa Ridhiwani uliopelekea serikali kutoa kiasi cha shilingi Bilioni 1.8 kwa ajili ya ujenzi wa Mabwawa mawili makubwa ya Maji katika Kitongoji cha Mjema na jengine kijiji cha Kwa-Msanja ambayo yatasaidia kupeleka maji na kumaliza changamoto ya maji kwenye Vijiji vya Kata Ya Kibindu hususan Kwa- Mduma, Kibindu, na kitongoji cha Kwa-Vuli.