Meneja wa Wakala huo
Mkoani Tanga Mhandisi George Tarimo akizungumza jambo wakati wa mafunzo | Meneja wa Wakala huo
Mkoani Tanga Mhandisi George Tarimo akizungumza jambo wakati wa mafunzO kuhusu mfumo wa Termis wa ukusanyaji
wa tozo za maesho kwa njia ya Kidigitali kwa waandishi wa habari mkoani Tanga |
| Meneja wa Wakala huo
Mkoani Tanga Mhandisi George Tarimo akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo |
| Meneja
wa Wakala huo
Mkoani Tanga Mhandisi George Tarimo akizungumza wakati wa mafunzo hayo
kushoto ni Meneja wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene |
| Meneja
wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene akieleza jambo
wakati wa mafunzo hayo kulia ni Meneja wa Tarura Mkoa wa Tanga Mhandisi
George Tarimo |
| Mchambuzi wa Mifumo Joseph Chigalula akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo |
| Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Sussan Uhinga akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo |
| Ufafanuzi ukiendelea kutolewa |
| Mwandishi wa TBC Mkoa wa Tanga Bertha Mwambele akizungumza wakati wa mafunzo hayo |
Sehemu ya watumishi wa Tarura wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mafunzo hayo A OSCAR ASSENGA, TANGA. WAKALA wa Barabara za Vijijini
na Mijini nchini (Tarura) mkoani Tang umetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo
waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu mfumo wa Termis wa ukusanyaji
wa tozo za maesho kwa njia ya Kidigitali huku wakitakiwa kuwa mabalozi. Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Meneja wa Wakala huo
Mkoani Tanga Mhandisi George Tarimo alisema mfumo huo sio mpya nchini
kwani umeshatekelezwa mikoa mengine huku akiwataka wananchi kutoa
ushirikiano . Alisema kwa maana mfumo huo sio mpya hapa nchini
kwani umeshatekelezwa mikoa mbalimbali lengo kubwa la serikali ni
kuhakikisha unatumika nchi nzima na wataalamu watakuwa wakitoa elimu. Aidha
alisema mfumo huo ni rafiki na rahisi ambao unawezesha mapato ya
Serikali kuweza kufika sehemu husika tofauti na awali maana watakuwa
hawapokei fedha mbichi kwani wenye chombo watakuwa wakilipa wenyewe kwa
simu na fedha yako inafika kwenye mfuko mkuu wa serikali na baadae
kurejeshwa kutengeneza barabara. “Kwa kweli mfumo huu ni mzuri
kwani ni rafiki na rahisi ambao utawezesha mapato ya Serikali kuweza
kufika sehemu husika tofauti na awali na baadae kurejeshwa kutumika
katika kuimarisha miundombni ya barabara”Alisema Alisema kwenye
mfumo huo mpya wa tozo za ukusanyaji wa maegesho awali Tanga walikuwa
wakikusanya tozo za maegesho za magari lakini kwa sasa kutokana na mfumo
na kanuni za utunzaji wa maegesho zilizotoka mwaka jana zinawataka
kutoza tozo za maegesho kwenye pikipiki na vyombo vya magairi matatu
bajaji na viwango vimebadilika. Aidha alisema awaIi walikuwa wanachaji kwa siku kwenye
magari kwa gari kwa sasa ambapo kuna vifurushi vya aina nne kwa saa 300
na siku nzima 1000 huku wiki ikiwa ni 5000 na magesho kwa mwezi 20000. Hata hivyo alisema kwa upande wa pikipini kwa siku 300 na kwa wiki
itakuwa 1500 wakati itakuwa ni mwezi 6000 ikiwemo kueleza kwa pikipiki
zenye magurudumu matatu (Bajaji) kwa siku 500,wiki 2500 na mwezi 20000. Hata
hivyo alisema kwa mujibu wa hiyo kanuni limewataka kutekeleza zoezi la
ukusanyaji kwa halmashauri za miji na wamejipanga kwenye Halmshauri za
Korogwe mjini na Handeni Mjini ila huko viwango vitakuwa tofauti. “Niwaase
wananchi wa Mkoa huu na viunga vyake kutoa ushirikiano ili wasikute
wanachajiwa vifurushi ambacho hukustahili kuchajiwa na zoezi hilo
litafanyika kuanza saa 12 hadi saa kumi na mbili jioni kwa Jumatatu
hadi Ijumaa huku Jumamosi litaanza 12.00 hadi saa saba mchana”Alisema “Usikubali kutozwa zaidi ya saa saba siku ya Jumamosi lakini Jumapili hatufanyi kazi na siku za sikukuu”alisema Hata
hivyo aliwasihi wananchi wa mkoa wa Tanga watoe ushirikiano pale ambapo
watakapopata changamoto kwa sababu ni mfumo mpya hivyo wasisite kufika
kwenye ofisi zao na wale wanaotoza kwa njia ya kidigidali wamepewa
mafunzo. “Kwa kipindi chote tutakapokuwa Tanga wataalamu
watakuwa katika maeneo ya Msingi kutoa taarifa na kuelekeza wananchi na
wadau zoezi hilo litakuwa endelevu hadi hapo watakapokuwa na uelewa wa
pamoja lengo ni wananchi waifurahi hiyo huduma “Alisema |