Mkuu wa mkoa wa Tabora ,Balozi Dkt Batilda Burian alipokuwa akifungua semina ya kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za mawasiliano kilichoitishwa na baraza la watumiaji wa huduma za mawasiliano TCRA CCC
Katibu Mtendaji wa barara la ushauri wa huduma za mawasiliano TCRA CCC Mary Msuya akizungumza na wadau wa mawasiliano katika semina ya kuelimisha na kushauriana na watumiaji wa huduma za mawasiliano.
Wanansemina wa kimsikiliza mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Burian
……………………………………………….
Na Lucas Raphael, Tabora
Wananchi mkoani Tabora wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kutangaza Fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla .
Wito huo ulitolewa na Mkuu wa mkoa wa Tabora ,Balozi Dkt Batilda Burian alipokuwa akifungua semina ya kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za mawasiliano kilichoitishwa na baraza la watumiaji wa huduma za mawasiliano TCRA C CC kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha veta mkoni hapa
Alisema kwamba mitandao ya kijamii itumike vizuri kutanga fursa zilijitokeza zilizopo mkoani tabora ili ziweze kuwa chanchu ya mafanikio kwa maendeleo ya jamii husika
Alisema kwamba sekta ya mawasiliano ikitumika vizuri ina wezesha utoa huduma bora na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi na wananchi wenyewe kutumia huduma hiyo kwa ajili ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi ,kielimu na kijamii.
Alisema kwamba wananchi wanapaswa kutumia fursa zinazotokanazo na huduma za kujiongezea taarifa za masoko ,uzalishaji mali ,elimu na huduma nyingine za maendeleo ya jamii yote.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa akizungumzia mafanikia ya mawasiliano alisema kwamba “bado kuna changamoto katika sekta zinazohitaji ushirikiano kwa wadau wote yaani serikali ,mamlaka ya mawasiliano ,Brazara la watoa huduma na watumiaji wa huduma katika kuzitatua ‘alisema balozi Dkt Buriani.
Alisema kwa sasa kunatatizo la wizi wa kimtandao ,matumizi yasio sahihi ya Internet na mitandao ya kijamii ambayo yamekuwa yakijitokeza kila uchao kwa jamii yetu.
Balozi Dkt Buriani alilishauri barara la ushauri wa huduma za mawasiliano kuhakikisha watumiaji wa huduma za mawasiliano kuweka mikakati madhubuti katika kufanya utafiti juu ya matatizo na kero za watumiaji pamoja na kutoa mashauri ya mara kwa mara na wadau wote ii kuondoa kero zinajitokeza .
Awali katibu Mtendaji wa barara la ushauri wa huduma za mawasiliano TCRA CCC Mary Msuya alisema kwamba wamejiwekea mikakati ya kuelimisha na kushauriana na watumiaji wa huduma za mawasiliano ili watambue haki ,wajibu ,sheria na maswala mazima ya watumiaji.
Alisema kwamba baraza litaendele kuelimisha umma wa watanzania katika masuala ya mawasiliano kwa jamii inayopata huduma za mitandao mbalimbali ya kijamii.
Hata hivyo katibu mkuu huyo aliwataka wananchi kuacha uharibifu wa miundombinu kwani kuharibu kunaisababaishia serikali fedha nyingi kuirejesha iweze jambo ambalo litawakwamisha wananchi kupata huduma za mawasiliano kwa wakati.