Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi ) Balozi Aisha Amour akizungumza na baadhi ya wananchi wakisubiri kupata huduma ya vivuko mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa utoaji huduma za vivuko Magogoni leo tarehe 05/03/2022 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi ) Balozi Aisha Amour akiongozana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Lazaro Kilahala kukagua maeneo ya utoaji huduma za vivuko Magogoni mara baada ya kufanya ziara ya kikazi leo tarehe 05/03/2022 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi ) Balozi Aisha Amour akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa utoaji huduma za vivuko Magogoni leo tarehe 05/03/2022 Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi ) Balozi Aisha Amour akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa utoaji huduma za vivuko Magogoni leo tarehe 05/03/2022 Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi ) Balozi Aisha Amour akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Lazaro Kilahala mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa utoaji huduma za vivuko Magogoni leo tarehe 05/03/2022 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wakifanya huduma ya malipo kwa kutumia kadi za kielektoniki kwenye eneo la vivuko Magogoni leo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Balozi Aisha Amour amefanya ziara ya kutembelea na kukagua huduma za vivuko Magogoni Jijini Dar es Salaam na kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu huduma zitolewazo katika eneo hilo.
Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi Balozi Aisha amesema kutokana na uwepo wa msongamano mkubwa wa abiria wakisubiri kupata huduma hiyo, Serikali itatenga fedha za manunuzi ya kivuko kingine na kuwa vitano katika eneo hilo.
Amesema ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuboresha huduma za kwenye maji pamoja na kupunguza msongamano wa abiria na magazine kwenye eneo hilo.
“Tunatarajia baada ya kivuko hicho kuwasili, kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 500 Sawa na abiria 2,000 na magari 60 na tayari fedha zimeshatengwa kwenye bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2022/23”. Amesema Balozi Aisha.
Nae Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Lazaro Kilahala alisema serikali imefanya maboresho ya ukataji tiketi kwa kusimika mfumo mpya wa kielekroniki (N-CARD) wa kusimamia mapato katika eneo hilo.
“Mfumo huo unaondoa mfumo wa zamani wa kutumia tiketi za karatasi na tayari tumeona mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa abiria katika sehemu ya kukatia tiketi,” alisema Kilahala.
Ameongeza kuwa abiria ambao wanatumia kivuko hicho kwa nadra wamewekewa utaratibu wa kadi za muda watakazozitumia wakati wa kuvuka katika eneo hilo.
Pamoja na hayo Mhandisi Kilahala amesema kivuko cha Mv.Kazi kimepelekwa kwenye matengenezo na kinatarajiwa kuanza kufanya kazi miezi mitatu ijayo.