Baadhi baaadhi ya wajumbe wa Alat Mkoa wa Pwani wakiwa na Mwenyekiti wao mpya Mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
…………………………………………………………
Na Victor Masangu,Kibaha
Jumuiya ya Tawala za mitaaa Tanzania((ALAT) Mkoa wa Pwani imefanikiwa kupata mwenyekiti wake mpya baada ya kupitishwa kwa kishindo bila kupingwa kwa kupata kura 35 za ndio.
Mwenyekiti huyo aliweza kupitishwa na wajumbe hao katika nafasi hiyo kutokana na kuwa peke yake katika nafasi hiyo hivyo kufanikiwa kushika nafasi hiyo ambayo ilikuwa wazi.
katika mkutano huo ambao ulihudhiliwa pia na wajumbe wa Alat Mkoa wa Pwani ambao baadhi yao ni wakurugenzi wa halmashauri,madiwani pamoja na wenyeviti wa halmashauri mbali mbali.
Awali akifungua mkutano huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Mwanasha Tumbo amewataka viongozi hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwemo suala zima la kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo.
Alisema kwamba wenyeviti na wakurugenzi wa Halmashauri zote wanapaswa kuweka mipango madhubuti ya kuibua na kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi.
Pia aliwaomba waendelee kuwaelimisha wananchi katika suala zima la kupambana na wimbi la ugonjwa wa Uviko-19 na kuwahamasisha waweze kuchanja.
“Ninawaomba viongozi wa Alat Mkoa na wakurugenzi kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuchanja ili kuepukana na ugonjwa wa Uviko-19 ikiwa sambamba na kuwahimiza wananchi katka zoezi zima la kufanya sensa na makazi,”alisema Mwanasha.
Naye Mwenyekiti mpya wa Alat Mkoa wa Pwani Ligomba aliahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali na viongozi wenzake kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika sekta mbali mbali.
Kadhalika aliahidi kutatekeleza maagizo yote ambayo yametolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani ikiwemo suala la anuani za makazi,sensa,kubuni vyanzo vipya vya mapato na mapambano dhidi ya ugonjwa wa uviko-19.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde alisema kwamba kwamba kwa upande wao wamejipanga vilivyo kuongeza vyanzo vipya vya mapato ikiwemo mradi wa soko kubwa la kisasa.