Shabiki wa Yanga na timu ya Chelsea, Peter Nangi akipozi baada ya kuzawadiwa mfano wa hundi baada ya kufanikiwa kubashiriki kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali duniani. Nangi alizawadiwa Sh50 milioni
************************
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Kampuni ya mchezo ya kubahatisha ya M-BET Tanzania imezidi kumwaga fedha baada ya kumzawadia shabiki wa timu ya Yanga na Chelsea Peter Nangi kitita cha Sh milioni 50.
Nangi ambaye ni mkazi wa Geita, ameshinda kiasi hicho cha fedha baada ya kubashiri kwa usahihi jumla ya michezo 12 ya mchezo wa kubahatisha wa Perfect12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania.
Mkurugenzi Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa Nangi ameibuka mshindi ikiwa siku moja tu baada ya Shabiki wa klabu ya Simba na Arsenal Swalehe Enzi ameshinda kitita cha sh 176,470,910 kupitia pia Perfect12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania.
“ M-Bet sasa imeanzisha kampeni mpya inayoitwa ZALI LA M-BET ambapo ukicheza na M-Bet unaweza jishindia Pikipiki na pesa taslimu kila wiki huku Mwishio wa kampeni mshindi mmoja ataondoka na Toyota IST,” Mushi.
Kwa upande wake, Nangi alisema kuwa ushindi wake umetokana na kuwa makini katika kuchagua timu bila ya kufauata alama za ushindi ambazo kila timu imekuwa ikipewa katika mkeka.
Alisema kuwa alianza kubet miezi sita iliyopita na ushindi huu umempa faraja kubwa sana kwani ataongeza mtaji wake na kujishughulisha zaidi na kilimo.
“Siri kubwa ya kushinda bahati nasibu hii kujua uwezo wa timu pamoja na kufanyia utafiti wa timu, aina ya wachezaji ambao wamesajili, aina ya timu unayocheza nayo pamoja na majeruhi.
Ukibet kwa kupenda timu yako, unapotea kwani lazima uwe mfuatiliaji wa michezo mbalimbali. Kama unajua inafungwa, tabiri hivyo na weka mapenzi pembeni kwenye shughuli hii,” alisema Nangi.
Mwisho….