…………………………………………………..
Na Lucas Raphael,Tabora
Wakala wa Mbegu za Kilimo wametoa ufafanuzi kwamba ASA haizalishi Mbegu zenye vinasaba vilivyobadilishwa (Genetically Modified Organism- GMO) bali uzalisha Mbegu za Uchavushaji huru (Open Pollinated Varieties-OPV) na mbegu chotara (Hybrid) kwa mazao mbalimbali yanayolimwa na wakulima walio wengi Nchini.
Kauli hiyo ilitolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) Dkt. Sophia Kashenge alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya matumizi ya mbegu bora za mazao mbalimbali yanayozaliswa na Taasisi hiyo
Alisema kwamba Wakala wa Mbegu (ASA) umejikita zaidi katika kuzalisha Mbegu za Uchavushaji huru (Open Pollinated Varieties-OPV) na mbegu chotara (Hybrid) kwa mazao mbalimbali yanayolimwa na wakulima walio wengi Nchini.
Alifafanua zaidi, alisema kwamba sehemu kubwa ya Mbegu zinazozalishwa na Wakala ni zile za OPV kwa kuwa zinampa mkulima uwezo wa kuzitumia tena kwa msimu mmoja zaidi au miwili kama hana uwezo wa kununua Mbegu Mpya.
Alisema kuwa Mbegu za OPV mbali na kuwa na sifa ya kustahimili Mazingira mengi Nchini, hutumika na wakulima wengi na bei yake ni nafuu na kila Mkulima anauwezo wa kununua.
Dkt Kashenge alisema, uwepo wa mbegu chotara unampa mkulima chaguo la kuweza kununua tena mbegu kwa msimu mwingine wa kilimo.
Dkt Sophia Kashenge amesema Mbegu chotara zinatoa mavuno mengi hasa pale Mkulima akifuata taratibu za Kilimo Bora huku akiongeza kuwa ilimkulima anufaike Vizuri ni budi kununua kila msimu na kuhakikisha taratibu za uzakishaji zinafuatwa
Alisema Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) Kama Taasisi ya Serikali inahakikisha wakulima wote kupata Mbegu Bora zilizo kidhi viwango vya ubora
Mtekenelojia wa Mbegu za kilimo (ASA) Grace Matina alisema kwamba wakulima wengi hawajui adhari za GMO ambazo uharibu na kubadilisha jenetikia ya mazao ya Mbegu .
Grace alisema madhara mengine ni Ongezeko la Magugu yanayo athiri mimea ambapo zinaweza kuleta mimea ambayo haikuwepo hali inayosababisha madhara mengine ya kiafya.
Grace alisema kwamba madhara hayo ambayo serikali ilishaweka katazo kubwa kwa Mbegu hizokwa kuandalia afya za watumiaji pamoja na uharibifu wa mazingira ambao unaweza kujitokeza.
Alisema kwamba aidha ni muhimu kufanya utafiti ili kubaini madhara na faida ili kufanya maamuzi sahihi kwa baadaye
Hivi karibuni Naibu Waziri wa kilimo Antony Mavunde alifanya ziara ya kikazi kwa Wakala wa Mbegu na kuwataka kuzalisha Mbegu kwa wingi na kwa ubora mkubwa ilikuepusha malalamiko ya wakulima kukosa Mbegu.
Mavunde alisema Kama serikali itandelea kuongeza bajeti katika Taasisi hiyo iliwaweze kuzalisha Mbegu zote wanazo hitaji wakulima.
Waziri Mavunde akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo aliwataka waendelee kufanya kazi kwa kujituma iliwaweze kukidhi mahitaji ya wakulima.