Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akisikiliza taarifa ya ujenzi wa chuo cha VETA cha Wilaya ya Chemba (Chemba DVTC) Mkoa wa Dodoma ikisomwa na Mkuu wa chuo cha VETA Mkoa wa Dodoma Bw.Stanslaus Ntibara mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa chuo cha VETA cha Wilaya ya Chemba (Chemba DVTC) Mkoa wa Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chemba Simon Chacha wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo cha VETA cha wilaya ya Chemba (Chemba DVTC) Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Chemba Mh Mohammed Moni wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo cha VETA cha wilaya ya Chemba (Chemba DVTC) Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dk.Pancras Bujulu wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo cha VETA cha wilaya ya Chemba (Chemba DVTC) Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akeiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa chuo cha VETA cha Wilaya ya Chemba (Chemba DVTC) Mkoa wa Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho.
MUONEKANO wa wa majengo ya ujenzi wa chuo cha VETA cha Wilaya ya Chemba (Chemba DVTC) Mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akizungumza na wananchi wa Bahi wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa chuo cha VETA cha Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa Chuo cha VETA wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akizungumza Mbunge wa Jimbo la Bahi, Mhe. Kenneth Nollo, akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa Chuo cha VETA wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa ujenzi wa chuo cha VETA cha Wilaya ya Bahi Mkoani wa Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda wakati akitoa maelezo kwa mkandarasi wa ujenzi wa Chuo cha VETA wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akikagua ujenzi wa Chuo cha VETA wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma.
MUONEKANO wa Chuo cha VETA wilayani Bahi Mkoani Dodoma.
…………………………………………
Na Alex Sonna-CHEMBA,BAHI
NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, ameitaka Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA),kukaa na viongozi katika uandaaji wa kozi zitakazofundishwa kulingana na mahitaji ya maeneo husika.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa vyuo vinavyojengwa kwa gharama ya Sh. Bilioni 2.2 kwa kila kimoja katika Wilaya za Chemba na Bahi mkoani Dodoma.
Amesema Sera ya Taifa sasa ni kujenga chuo kila wilaya ili kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi waweze kunufaika na mafunzo na kwamba walianza na wilaya 29 ambapo wilaya nne ujenzi umekamilika.
Kipanga amesema ujenzi wa vyuo hivyo unafanyika katika halmashauri na wilaya ambapo kuna viongozi kwenye maeneo hayo na hivyo ni muhimu wakashirikishwa katika kila hatua.
“Hata mazingira ya Chemba na Bahi wao ndio wanafahamu hata aina gani ya kozi kwamba ni kozi gani ikitolewa itawafanya kutoka katika hali waliyonayo na kwenda mahali pazuri zaidi,”amesema.
Ametaka suala la uchambuzi wa kozi zitakazotolewa na vyuo hivyo wasilitoe wao wenyewe makao makuu bali wawashirikishi watu wa maeneo husika
“Tunaleta Chuo cha Veta hapa lakini wanaojua mazingira ya Veta ni hawa wananchi kwa hiyo hata kozi zitakazotakiwa hapa ni wao wanazifahamu wanajua kozi hizi zikitolewa tutatoka hapa tulipo, uanzishaji wa kozi ufanyike kikao cha pamoja nendeni kwenye mabaraza ya Madiwani mpokee mawazo yao kuhusu kozi bora zitakazosaidia,”amesema Kipanga
Kwa upande wao Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Chacha na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda,amesema watashirikiana na Veta kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa katika ujenzi huo zinatumika kwa kadri maelekezo ya Serikali.
Awali, Mkuu wa Chuo cha VETA mkoani Dodoma, Stanslaus Ntibara, amesema kuwa wanafunzi 300 watadahiliwa kwenye fani sita za muda mrefu baada ya kukamilika kwa ujenzi huo huku kwa mafunzo ya muda mrefu wanakadiria wanafunzi kati ya 250 hadi 400 kudahiliwa kwa mwaka.
Naye, Mbunge wa Bahi, Kenneth Nollo na Mbunge wa Chemba Mohamed Moni,amesema kuwa vyuo hivyo vina uwezo mkubwa wa kubadilisha maisha ya watu na kwamba bado kuna kazi kubwa ya kuhakikisha kunakuwa na wahitimu wengi wa vyuo vya ufundi kuliko wale wa shahada.
‘Tunaiomba Serikali kuhakikisha kuwa wanafunzi wa kutoka wilaya hizo mbili wanapewa kipaumbele kwenye vyuo hivyo”wamesema