Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akizungumza na Wananchi wa Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya katika Mkutano uliofanyika leo katika viwanja vya CCM Machi 1, 2022, Wananchi hao walimpongeza Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akisalimiana na wananchi wa Tukuyu baada ya kuzungumza nao katika Mkutano uliofanyika leo viwanja vya CCM Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, Machi 1, 2022, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mhe. Dkt. Vicent Anney. Wananchi hao walimpongeza Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Mbunge wa Busokelo, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete akizungumza na Wananchi wa Tukuyu Wilayani Rungwe katika Mkutano uliofanyika leo katika viwanja vya CCM Mkoani Mbeya,
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mhe. Dkt. Vicent Anney akizungumza na Wananchi wa Tukuyu Wilayani Rungwe katika Mkutano uliofanyika leo katika viwanja vya CCM Mkoani Mbeya
Mbunge wa Rungwe, Mhe. Anthony Mwantona akizungumza na Wananchi wa Tukuyu Wilayani Rungwe katika Mkutano uliofanyika leo katika viwanja vya CCM Mkoani Mbeya,
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mhe. Suma Fyandomo akizungumza na Wananchi wa Tukuyu Wilayani Rungwe katika Mkutano uliofanyika leo katika viwanja vya CCM Mkoani Mbeya,
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mhe. Sophia Mwakagenda akizungumza na Wananchi wa Tukuyu Wilayani Rungwe katika Mkutano uliofanyika leo katika viwanja vya CCM Mkoani Mbeya.
Wananchi wa Tukuyu Wilayani Rungwe wakimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mb (hayupo kwenye picha) akizungumza katika Mkutano uliofanyika leo katika viwanja vya CCM Mkoani Mbeya, Machi 1, 2022, Wananchi hao walimpongeza Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
………………………………………………
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson ( Mb), amewaasa wananchi wa Tukuyu Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya kuacha kutumia muda mwingi kujadili siasa badala yake waelekeze nguvu na maarifa katika miradi itakayowaletea maendelo.
Mhe. Spika ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika leo tarehe 1 Machi, 2022 Wilayani humo kwa lengo la kumpongeza kuchaguliwa kwake kuwa Spika wa Bunge.
Pamoja na kuwashukuru wananchi hao kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo, Mhe. Spika amemshukuru Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia mchakato wa kupitisha jina lake na kugombea nafasi hiyo.
“Hii nafasi tusingeweza kuipata bila yeye lakini shukrani zetu zinakwenda mbali zaidi ya hapo. Katika wingi wa mambo aliyoyafanya, sisi kama Wananchi wa Rungwe lazima tumshukuru kwa miradi mbalimbali inayoendelea katika maeneo yetu. Sekta ya elimu hapa ameleta zaidi ya shilingi billioni 1.1 ili madarasa yajengwe kwenye shule zetu za sekondari watoto wetu waweze kusoma. Rais wetu haupigi mwingi huko kwingine pekee bali anaupiga mwingi hadi hapa kwetu Rungwe” ameongeza Dkt. Tulia
Aidhaa, amewaeleza Wananchi hao kuhusu miradi mingine mbalimbali iliyofanywa na Serikali katika sekta ya afya na miundombinu, ambapo pia amewataka kuendelea kushikamana pasipokufuata mihemko ya kisiasa kwakuwa.
Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya kupitia CHADEMA Mhe. Sophia Mwakagenda amesema kuwa licha ya tofauti zao za kichama lakini anampongeza Mhe. Spika pamoja na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwakuwa wamekuwa ni Viongozi bora na wa mfano katika taifa na dunia kwa ujumla.
“Mheshimiwa Spika wewe ni Spika wa vyama vyote, mimi ni mmoja wa Wabunge wako ambao tulikuchagua kwa kura zote. Wakati tunakujadili tulisema hatuangalii chama bali tunaangalia akili na uwezo wa mtu” alisema Mhe. Mwakagenda
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe Ndg. Mpokigwa Mwankuga, amempongeza Mheshimiwa Dkt. Tulia kwa jitihada zake binafsi za kujitolea kwa jamii yake huku akitoa rekodi ya baadhi ya mambo aliyoyafanya ndani ya Halmashauri hiyo licha ya kwamba sio Mbunge wa eneo hilo.
“Katika rekodi ambayo Halmashauri hii imeweza kuzirekodi kwa wewe binafsi kujitolea katika sekta mbalimbali hadi sasa ni zaidi ya shilingi 1.13 bilioni Mheshimiwa Spika fedha hizi ungeweza kuzipeleka kwenye familia yako lakini uliamua kuwasaidia wana-Rungwe ili kuhakikisha wote wanapata maendeleo, tunakushukuru sana” alisema Mwankuga