Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akisikiliza taarifa ya mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma ikisomwa na Mshauri mwelekezi wa mradi Aliki Nziku,wakati wa ziara ya Naibu Waziri ya kukagua ujenzi wa chuo hicho jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akikagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma kinachojengwa eneo la Nala jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akitoa maelezo kwa wasimamizi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma kinachojengwa eneo la Nala jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akimsikiliza Meneja wa Mradi Bw.Gao Yuqi wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma kinachojengwa eneo la Nala jijini Dodoma.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma kinachojengwa eneo la Nala jijini Dodoma wakiendelea na ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma kinachojengwa eneo la Nala jijini Dodoma.
Meneja wa Mradi Bw.Gao Yuqi,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga kumaliza kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma kinachojengwa eneo la Nala jijini Dodoma.
Mshauri mwelekezi wa mradi Aliki Nziku,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga kumaliza kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma kinachojengwa eneo la Nala jijini Dodoma.
Muonekano wa ujenzi wa Shule ya mfano inayojengwa eneo la Iyumbu jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akikagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya mfano inayojengwa eneo la Iyumbu jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi wa maendeleo ya ujenzi wa Shule ya mfano inayojengwa eneo la Iyumbu jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
Operesheni Kamanda wa mradi huo kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Philemon Komanya,akielezea ujenzi wa shule hiyo ulipofikia wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa maendeleo ya ujenzi wa Shule ya mfano inayojengwa eneo la Iyumbu jijini Dodoma.
………………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga,amesema kuwa Chuo cha Ufundi Dodoma(DIT) kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1500 kitakapokamilika huku akiridhishwa na kasi ya ujenzi wa chuo hicho.
Kipanga ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara ya kukagua Maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho inayojengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 17.9 kinachojengwa na Mkandarasi kutoka kampuni CRJE katika kijiji cha Lugala,Nala jijini Dodoma.
Amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa chuo hicho kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1500 pindi kitakapokamilika huku akiridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi huo.
“Baada ya hiki cha Dodoma, tunajenga pia Arusha Chuo kikubwa cha mfano wa hichi ambacho pia kitagharimu zaidi ya Sh.Bilioni 17, tunajenga Centre of Excellence katika nishati Jadidifu, uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji, lengo ni kuhakikisha mafundi wa masuala ya uzalishaji wa umeme kwa njia ya maji tunaweza kuwazalisha wenyewe kama nchi,”amesema
Kipanga amebainisha kuwa kwa Dar es salaam kinajengwa kituo kwenye chuo cha DIT ambapo Sh.Bilioni 39 zimepelekwa kwa ajili ya kituo hicho ambapo itakuwa ni kwa ajili ya masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA).
“Kitakuwa chuo kikubwa kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati lakini ukienda NIT inajengwa Centre of Excellence kwenye masuala ya usafirishaji wa anga na majini, kwa mara ya kwanza katika nchi yetu tutazalisha marubani wetu wenyewe.”
Amesema kuwa Wizara itasimamia ujenzi wa vyuo hivyo kwa kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kunakuwepo wataalamu wa kutosha katika ulimwengu wa viwanda.
“Serikali yetu ya awamu ya sita imejikita sana kwenye upanuzi wa elimu hii ya kati yaani elimu ya ufundi, kwa hiyo vyuo hivi ni mfano wa vyuo vinavyojengwa katika Wilaya, tutajenga kila Wilaya nchini chuo cha VETA’amesema
Aidha ameeleza kuwa kwasasa wanamalizia ujenzi wa vyuo hivyo katika Wilaya 25 vingine vimeshakamilika na kuanza kutoa huduma.
“Lengo la serikali ni kushusha elimu ya ufundi katika maeneo yote nchini, na kuhakikisha kwamba watanzania wanahitaji ujuzi, ufundi wa kutenda zaidi kuliko elimu ile ya nadharia,”amesema Kipanga.
Mhe.Kipanga amesema kuwa ujenzi wa chuo hicho ulianza Juni 2021 inatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu makusudio yetu kama serikali ifikapo januari 2023 tuanza udahili hapa, iwapo tukikamilisha mjengo yote chuo kwa awamu ya kwanza kitakuwa na uwezo wa kuweka wanafunzi 600,watakaoishi chuoni,kitakapokamilika kwa ujumla kinatakiwa kuchukua wanafunzi 1500.
Awali Mshauri Mwelekezi wa mradi huo Bw.Aliki Nziku, amesema kuwa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 38 na kiasi cha Sh.Bilioni 3.9 zimelipwa.
Kwa upande wake Meneja wa mradi huo kutoka kampuni ya CRJE Gao Yuqi,amesema kuwa watahakikisha wanatekeleza mradi huo kwa viwango na kwa wakati kulingana na matakwa ya mkataba.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kipanga ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Mfano iliyopo Iyumbu Jijini Dodoma huku akipongeza kasi ya ujenzi huo unavyoendelea na kuwasisitiza kuendelea na kasi hiyo ili waweze kumaliza mapema.