Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),Titus Kaguo,akizungumza na waandishi wa habari leo March 1,2022 jijini Dodoma wakati akitangaza bei Mpya za Mafuta.
…………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei za mafuta ya Petroli,Diseli na Mafuta ya taa kwa mwezi Machi 2022 ambapo bei za rejareja za Dizeli na Petroli zimeongezeka kwa shilingi 60 kwa lita (sawa na asilimia 2.42) na shilingi 65 kwa lita sawa na asilimia 2.77 mtawalia.
Imesema bei hizo zingeweza kuwa juu zaidi kama Serikali isingechukua hatua ya kuahirisha tozo ya shilingi 100 kwa lita kwenye bidhaa za mafuta ya petrol,dizeli na mafuta ya taa.
Akitangaza bei hizo leo Machi mosi,2022mbele ya Waandishi wa Habari,Jijini Dodoma Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA,Titus Kaguo amesema bei za rejareja na jumla za mafuta hayo yaliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es salaam zimebadilika ikilinganishwa na toleo lilopita la Februari 2 mwaka huu.
Amesema hizo bei za rejareja za Dizeli na Petroli zimeongezeka kwa shilingi 60 kwa lita (sawa na asilimia 2.42) na shilingi 65 kwa lita sawa na asilimia 2.77 mtawalia.
Amesema bei ya rejareja ya mafuta ya taa imepungua kwa shilingi 83 kwa lita sawa na asilimia 3.63.
“Vilevile ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita bei za jumla za petrol na dizeli zimeongezeka kwa shilingi 59.65 kwa lita sawa na asilimia 2.54 na shilingi 64.45 kwa lita sawa na asilimia 2.95 mtawalia.
Amesema bei ya mafuta ya taa imeshuka kwa shilingi 82.67 kwa lita sawa na asilimia 3.82.
Amesema bei za mafuta hayo kwa Mikoa ya Kaskazini (Tanga,Kilimanjaro,Arusha na Manyara zimeongezeka ikilinganishwa na bei zilizotolewa Februari 2 mwaka huu.
Amesema kwa Machi,2022 bei za rejareja petrol na diseli zimeongezeka kwa shilingi 165 kwa lita sawa na asilimia 6.88 na shilingi 207 kwa lita sawa na asilimia 9.09 mtawalia.
“Vilevile ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita bei za jumla na rejareja petroli na dezeli zimeongezeka kwa shilingi 164.76 kwa lita sawa na asilimia 7.26 na shilingi 206 kwa lita sawa na asilimia 9.62 mtawalia.