Naibu Waziri wa kilimo Antony Mavunde kulia aliyevaa kofia bluu akipata maelekezo ya Uzalishaji wa Mbegu kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA, Dkt Sophia Kashenge katika Maabara ya Wakala.
Naibu Waziri wa kilimo Mhe.Antony Mavunde kushoto akikagua na kuangalia uchakataji wa Mbegu katika Ghara la Wakala wa Mbegu za kilimo ASA kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Dkt.Jusitin Ringo akiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala Dr Sophia Kashenge wakitoa maelezo dhidi ya uchakataji wa Mbegu katika Ghara la Wakala Makao Makuu Morogoro.
………………………………………………………………
Na Lucas Raphael, Morogoro
Naibu Waziri wa kilimo Antony Mavunde amewaagiza Wakala wa Mbegu za kilimo ASA kuhakikisha Wana pata hati miliki ya Mashamba pamoja na kuyawekea uzio ili kuepusha Migogoro na uvamizi unaosababishwa na wakulima na wafugaji mkoani Morogoro
Alitoa kauli hiyo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi katika Shamba la Wakala mbegu wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro alisema Wakala wa Mbegu za kilimo ASA inapaswa kuanza mchakato wa kuyakatia hati miliki ya Mashamba yake yote sambamba na kuweka uzio.
Mavunde Alisema Wakala akikata hati miliki ya maeneo yake atapunguza Migogoro ya Aridhi dhidi ya wananchi wanaozunguka mashamba hayo kutokana na kuwa na hati miliki inayotambua mipaka yake.
Akizungumzia suala la kuweka uzio Wakala wa mbegu awapaswa kuweka uzio mashamba yake yote ili kuhepuka Migogoro isiyokuwa ya lazima na Wananchi wanaozunguka mashamba hayo.
Alisema hivyo kufuatia Taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wakala wa mbegu ASA Dkt, Sophia Kashenge kusema kwamba mashamba yamekuwa yakivamiwa na wafugaji kwa kuingiza mifugo shambani hali inayo hatarisha usalama wa Mbegu zinazozalishwa kwenye eneo hilo la msimba .
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt Sophia Kashenge akipokea maelekezo ya Naibu Waziri Antony Mavunde alisema maelekezo yote yaliyotolewa yatafanyiwa Kazi.
Alisema Wakala wa Mbegu itandelea kuhakikisha inafanya kazi kwa kuzingatia maelekezo ya Wizara ya Kilimo hasa katika kipindi hiki cha msimu wa Kilimo.
Dkt Sophia alisema serikali ya wilaya ya Kilosa kupitia Mkuu wa wilaya Alhaji Majid Hemedi Mwanga wamakuwa wakitoa ushirikiano Mkubwa ambao amekuwa akiufanya hasa katika kutoa Elimu kwa wananchi wanaozunguka mashamba hayo ya Wakala.
Alisema Wakala wa Mbegu inakua kwa kasi kubwa kwa sababu Mbegu ni biashara na Mbegu imepewa Mkazo mkubwa na serikali nakuongeza kuwa Wakala itandelea kuzalisha Mbegu bora.
Alisema malengo ya Wakala wa Mbegu nikuhakikisha Mbegu zote Zina patikana Nchini na kwa ubora wa kimataifa ili kuwafanya wakulima wapate kile wanachokitaka.
Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Alhaji Majidi Hemedi Mwanga aliwapongeza Wakala wa Mbegu za kilimo ASA kwa kuendelea kuzalisha Mbegu bora za kilimo katika Shamba la Msimba Kilosa Mkoani Morogoro.
Alisema Kama serikali ya wilaya itandelea Kushirikiana na Wakala katika kulinda maeneo yote na kuhakikisha wananchi hasa kundi la wafugaji kutovamia mashamba ya Wakala.