Katibu msaidizi wa Chama cha soka la wanawake Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya Ocede Queens baada ya kuutwaa ubingwa huo.
******************
Na Victor Masangu.
Timu ya soka ya wasichana ya Ocode Queens imefanikiwa kuutwaa ubingwa wa kinyang’anyiro cha michuano ya Nata Ocode start baada ya kuichapa timu ya JMK Queens kwa mabao 2-0.
Katika mchezo wa fainali hizo ambazo zilikuwa na ushindani na upinzani wa hali ya juu kutoka na wachezaji wa pande zote mbili kulisakata kabumbu kwa kiwango cha hali ya juu.
Wachezaji wa timu ya Ocode Queens walionekana kubadilika katika kipindi cha pili kwa kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa wapinzani wao ambayo yaliweza kuzaa matunda ya kuandika mabao hayo mawili yaliyodumu hadi kipenga cha kumaliza mchezo kinapulizwa.
Mara baada ya mchezo kumalizika nahodha wa timu ya Ocode Queens Kidawa Ally ally alilipongeza Shirika la Ocode kwa jitihada za kuweza kuanzisha programu ya mashindano hayo ambayo yameweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuinuana kukuza vipaji vyao katika sekta mchezo wa soka.
Aidha aliongeza kuwa wanaiomba serikali ya awamu ya sita kuweka mikakati endelevu ambayo itaweza kuwasaidia wasichana ambao ni wanafunzi waweza kupata fursa ya kukuza vipaji vyao katika mchezo huo wa kabumbu.
Kwa upande wake Meneja programu wa ustawi wa jamii kutoka Shirika la Ocode Dorice Matekele amebainisha kuwa wameanzisha programu hiyo ya mashindano ya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanafunzi wa shule mbali mbali zilizopo katika manispaa ya Ubungo lengo ikiwa ni kukuza mchezo soka.
Pia aliongeza kuwa programu hiyo uwa ufanyika kila mwaka mbapo kwa kipindi hiki umeshirikisha jumla ya timu nne ambazo zimepatiwa zawadi mbali mbali ikiwemo kupatiwa medani na vikombe na mchezaji Bora.
Naye Katibu msaidizi wa Chama cha soka la wanawake Mkoa wa Dar es Salaam Dkt.Cecilia Makafu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika fainali hizo amewataka wachezaji ili kufanikisha malengo yao inatakiwa wanapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu.