Kaimu Meneja Ufundi, Mhandisi Mathew Ndossi akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, kuhusu maboresho yaliyofanyika ya barabara ya kuruka na kutua ndege na maegesho katika Kiwanja cha Ndege Cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA), Mkoani Kilimanjaro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Kiwanja cha Ndege Cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA), Mkoani Kilimanjaro, wakati alipotembelea kiwanja hicho mkoani Kilimanjaro.
Meneja Tehama wa Kiwanja cha Ndege Cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA), Magati Munyambo, akimwonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, kifaa kinachotumika kutolea risiti za maegesho ya magari katika kiwanja hicho, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea kiwanja hicho Mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa kitengo cha Mizigo, Kiwanja cha Ndege Cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA), David Katondo, akifafanua kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, namna mizigo inavyotunzwa na kusafirishwa, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea kiwanja hicho Mkoani Kilimanjaro.
Mwongoza Ndege Mkuu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Norbeta Seneor akimwonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, kifaa kilichukuwa kinatumika kuandika taarifa za ndege, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) Mkoani Kilimanjaro.