………………………………………………
Kikosi cha KMC FC kimefanya maandalizi yake ya mwisho kuelekea katika mchezo wa kuanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania bara ambapo kesho itakuwa nyumbani ikiwakaribisha Timu ya Polisi Tanzania mchezo utakaopigwa saa moja kamili jioni (19:00) katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi Jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya Kocha Mkuu Thierry Hitimana imefanya maandalizi ya kutosha na kwamba kesho itaingia uwanjani ikihitaji ushindi wa kwanza kwenye mzunguko huu wa pili muhimu na kwamba kikosi kiko tayari kwa mtanange huo.
Aidha katika mchezo huo wa kesho kama Timu inafahamu ugumu wa mchezo huo utakavyokuwa kwani Polisi Tanzania ni Timu nzuri na kwamba licha ya ushindani huo utakaokuwepo lakini ubora wa wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Manispaa ya Kinondoni wamejipanga kupambania alama tatu muhimu kwani mchezo huo upondani ya uwezo wa KMC FC.
“ Tunakwenda kucheza na Polisi ni Timu nzuri, lakini KMC ni bora sana, pamoja na kuwa hatujawahi kuwa na matokeo rafiki pindi tunapokutana lakini awamu hii tutahakikisha tunashinda mchezo wetu, wachezaji wetu wote wapo vizuri ,wana hali nzuri na morali nzuri pia, kwa hiyo kikubwa tuombe uzima wachezaji wote wa amkesalama.
Siku zote unapohitaji mafanikio hakuna mapambano mepesi yote yanaushindani tena mkubwa, KMC tunahitaji matokeo kwa hali na mali, tunahitaji kuanza mzunguko wa pili wa kumaliza ligi vizuri, tunafahamu kila timu imejianda vema hivyo tupotayari kupambania Timu yetu, Manispaa yetu ilikupata matokeo mazuri sambamba kuendelea kuwa kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu.
Hata hivyo katika mchezo wa kesho KMC FC itawakosa wachezaji watatu ambao ni Golikipa Farok Shikalo ambaye alipata majeraha kwenye mazoezi, Kelvin Kijiri ambaye aliumika katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji pamoja na Miraji Athumani mambo ya kifamilia.
KMC FC inakwenda kuanza mzunguko wa pili na Kocha Mkuu Hitimana ambapo hadi sasa ameshahusika kwenye michezo mine katika duru ya kwanza ya Ligi Kuu ya NBC na kushinda michezo miwili ambapo kati ya hiyo mmoja ugenini na mmoja nyumbani, sare michezo miwili mmoja nyumbani na mwingine ugenini huku Timu ikiwa kwenye nafasi ya tisa (9) na kwamba malengo ni kufanya vizuri kwenye mzunguko wapili pamoja na kumaliza Ligi katika nafasi nzuri mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Imetolewa leo Februali 25