Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dk.Dorothy Gwajima akiwa katika mkutano na wadau mbalimbali mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika vituo vya ustawi wa jamii Kigamboni Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dk.Dorothy Gwajima akifurahi na baadhi ya watoto mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea madawati ya Jinsia Kigamboni Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dk.Dorothy Gwajima akipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea madawati ya Jinsia Kigamboni Jijini Dar es Salaam
*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Watumishi wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wametakiwa kuwa wabunifu na kupanga mikakati ya kuzuia vitendo vya ukatili badala ya kutegemea fedha kutoka kwa wadau ili watekeleze majukumu yao.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam katika ziara yake ya kikazi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dk.Dorothy Gwajima, amesema utekelezaji wa mkakati huo umeshaanza kufanyiwa tathimini na itahusisha sekta zote ambapo itafanya utaratibu wa kuwapeleka watoto hao shule na waliyoharibika kiafya na uvutaji wa madawa wapatiwe tiba.
“Serikali itakutana na wadau mbalimbali Februari 26 ili kuona mkakati gani uingie ambao utakuwa na maboresho na kuleta pendekezo la haraka litakalo husisha sekta zote katika kukabiliana na ili wimbi la watoto wa mtaani”. Amesema Waziri Gwajima.
Waziri Gwajima amesema Serikali itafanya tathimini kwa mujibu wa sheria kwa kuangalia sababu zilizowafanya watoto wawe katika mazingira hatarishi ambapo itaenda kuwajibisha wazazi wasiotekeleza majukumu yao.
Aidha Dkt.Gwajima ametoa wito kwa wazazi ambao wanajua watoto wao wapo mitaani kuhakikisha wanawachukua badala ya kusubiri kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.
“Kuna watoto waliokuwa mitaani kutokana na kutokuwajibika kwa wazazi tutaenda kuchambua sababu, tuangalie wamekuja kwasabubu ya nini wasifikili serikali itachukua tu watoto ili ni suala la pamoja”. Amesema.
Pamoja na hayo Dkt.Gwajima amesema katika kutokomez ukatili kwa wanawake na watoto amewataka watumishi wa ustawi na Maendeleo ya Jamii kushirikiana ipasavyo na kamati zinahusika na ulinzi wa watoto na wanawake kuanzia ngazi ya kata hadi mtaa ili kukabiliana na vitendo vya ukatili.
Vilevile amewataka watumishi wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi kutumia mbinu za kisasa katika kukutna na kamati na kujadili changamoto zilizopo katika jamii.