Kulia,
Mhandisi Mwinchuma Tengeneza akimkabidhi kablasha la eneo la kazi ya
Ujenzi na Ukarabati wa miundombinu, katika skimu ya kilimo cha
Umwagiliaji Idudumo mwakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya Explicit Main
Constructors Ltd Bw. Basil Clement (kushoto).
Picha Ikionesha eneo la Utoro wa Maji katika Bwawa la Idudumo ambalo litavunjwa na kujengwa upya.
Wapili
kutoka kulia, Meneja Mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa Skimu ya
Umwagiliaji Idudumo Bw. Juma Kibori akiwaonesha wawakilishi wa viongozi
wa Halmashauri ya Nzega mji na wataalam ramani ya ujenzi na ukarabati wa
eneo la mradi
Wakulima katika Halmashauri ya mji wa Nzega Mkoani Tabora,
wameonesha kuwa tayari na kutoa ushikiano kwa ujenzi na ukarabati wa
mradi wa kilimo cha Umwagiliaji Idudumo unaofadhiliwa na Serikali kwa
asilimia mia.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika
makabidhiano ya eneo la kazi katika skimu hiyo, Bw. Pascal Maganga
ambaye ni mkulima wa zao la mpunga katika skimu hiyo alisema, ujenzi na
ukarabati wa miundo mbinu katika skimu hiyoutasaidia wakulima kulima
zaidi ya mara moja katika misimu tofauti ya mvua,tofauti na sasa ambapo
ukosekanaji wa miundombinu unapelekea mashamba kujaa maji na kutokulima
kwa wakati na kuweza kuleta madhara kwa mazao.
“Naamini kuwa
baada yau jenzi na maboresho haya, kwa heka awali mkulima kama alikuwa
anapata gunia thelathini (30) ila baada ya maboresho haya tutavuna zaidi
.”Alise Mkulima huyo”Alisema
Akizungumza wakati wa makabithiano
hayo,Meneja mradi huo Mhandisi Juma Kibori kutoka Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji alisema eneo la skimu hiyo ya kilimo cha Umwagiliaji yenye
ukubwa Hekta 300, na kujikita zaidi katika kilimo cha mpunga chenye
chanzo chake cha maji ya Bwawa la Idudumo,lilikuwa likitumia njia za
asili na sasa itajengewa mfereji mkubwa wa kupeleka maji mashambani
wenye urefu wa mita 1500, vigawa maji sita, makaravati matano na
mifereji ya upili yenye urefu wa mita zaidi ya mia sita.
Aliendelea
kusema kuwa,awamu hiyo ya kwanza ya ujenzi na ukarabati wa skimu hiyo
utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 700, unaotegemea kuchukua miezi
nane,utaboresha miundombinu nakusaidia wakulima kuwa na kilimo cha
uhakika.