Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai akiotesha mti kama ishara ya kupokea msaada wa miche asili 2100 iliyotolewa na benki ya Absa Mjini Moshi huku Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa Absa Bank, Aron Luhanga (aliyechuchumaa kulia), Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Moshi, Pendo Abdallah (kushoto) na Afisa Mauzo, Baraka Haule.Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai (kulia) akishuhudia Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Absa Bank Aron Luhanga akiotesha mti kama ishara ya makavbidhiano ya miche 2100 iliyotolewa na benki hiyo kwa mkoa wa Kilimanjaro. Wengine kutoka kulia ni Meneja wa Absa Tawi la Moshi, Pendo Abdallah na Afisa Mauzo Saidi Borakupata.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai (kulia) akipokea moja ya miche iliyotolewa na Benki ya Absa kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Aron Luhanga (katikati). Kushoto ni Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Moshi Pendo Abdallah.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai akiotesha mti kama ishara ya kupokea msaada wa miche asili 2100 iliyotolewa na benki ya Absa Mjini Moshi huku Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa Absa Bank, Aron Luhanga (aliyechuchumaa kulia), Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Moshi, Pendo Abdallah (kushoto) na Afisa Mauzo, Baraka Haule.Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
*****************
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai ameipongeza benki ya Absa kwa mchango mkubwa inaotoa katika kuboresha mazingira hapa nchini ikiwemo mkoani humo.
Kagaigai ametoa pongezi hizo jana (Jumatano) wakati akipokea jumla ya miche 2,100 ya miti ya asili kutoka kwa uongozi wa benki hiyo, katika ofisi za Mkuu wa Mkoa, zilizoko Moshi.
“Kumekuweko juhudi kubwa zinazolenga kuboresha mazingira mkoani hapa, niwapongeze kwa mchango wenu huu muhimu na pia nitoe rai kwa taasisi zingine kuiga mfano wenu”, alisema.
Aidha aliupongeza uongozi wa benki ya Absa kwa kutoa miche ya miti ya asili ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa utunzaji wa vyanzo vya maji.
“Mkoa huu ndiyo nyumbani kwa Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote Barani Afrika, kuendelea kuweko kwake mlima huu ni vyanzo vya maji vihifadhiwe, hivyo miche ya miti ya asili itachangia katika utunzaji wa vyanzo hivyo muhimu”, alisema.
“Mlima Kilimanjaro ndiyo chanzo cha maji ambayo yanatumika kwa maswala mbalimbali ya kiuchumi kama vile uvuvi, kilimo, mazingira bora na matumizi aina mbalimbali kwa shughuli zinazofanywa na Binadamu, hivyo miti ya asili ni muhimu ili vyanzo vizidi kuhifadhiwa”, alisema.
Kagaigai pia alitoa rai kwa viongozi wa benki hiyo kuutangaza Mkoa wa Kilimanjaro kama mahali salama kwa uwekezaji ili kuinua hali ya kiuchumi ya Mkoa huo.
Kwa upande wake Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya Absa Aron Luhanga, amesema miche hiyo ya miti ni sehemu ya mchango wa benki hiyo ni sehemu ya mchango wao kwa jamii kupitia mashindano ya Kilimanjaro Marathon ambayo Benki ya Absa ibnadhamini kwa mwaka wa tatu sasa.
“Miche hii ni shukrani zetu kwa uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro ambao ulisaidia kwa benki yetu kuwa mmoja wa wadhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon mbazo hufanyika mkoani hapa kila mwaka kwa miaka 20 sasa”, alisema.
Alisema huu ni msimu wa tatu kwa benki hiyo kushiriki kama wadhamini wenza wa mbio hizo na kwamba ufadhili huo umechangia kwa benki hiyo kuwa sehemu ya familia inayochangia maboresho ya sekta ya michezo nchini.
“Leo tunatoa miche ya miti ya asili 2,100 ambayo inachangia kuhifadhi maji na hivyo kuchangia uhifadhi wa vyanzo vya maji; tunaahidi kuendelea kutoa mchango wetu mkubwa katika kuoboresha mazingira mkoani hapa”, alisema.
Katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa Kagaigai pamoja na Bw. Luhanga wa Absa Bank waliotesha miti ikiwa ni kumbukumbu ya makabidhiano hayo sambamba na uzinduzi wa upandaji wa miche hiyo ambayo itapandwa maeneo mbalimbali mkoani humo kama itakavyoagziwa na uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro.