WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ,akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga ,akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof. Caroline Nombo,akitoa taarifa ya wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
Wakuu wa vyuo mbalimbali wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akiangalia Kompyuta kabla ya kuzikabidhi kwa wakuu wa vyuo wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ,akiwakabidhi Kompyuta baadhi ya wakuu wa vyuo wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Marangu TC Dk.Colonel Chambulila,akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani) mara baada ya kukabidhi Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,DODOMA
WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa kupitia Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu nchini (Teacher Education Support Project (TESP) wameendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika Vyuo vya Ualimu ili kuongeza ubora wa elimu ,pamoja na kuwa na miundombinu rafiki kwa wanafunzi na walimu.
Hayo ameyasema leo Februari 21,2022 Jijini Dodoma wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa na wizara hiyo.
Amesema kuwa vyuo 13 vimepata Kompyuta 50 ambapo ,Vyuo 4 vimepata Kompyuta 30 na Vyuo 09 Kompyuta 20 na Vyuo vyote 35 vitapatiwa Kompyuta Mpakato moja kwa ajili ya kusaidia idara zingine vyuoni.
“Leo mtapatiwa Kompyuta za Mezani na Kompyuta Mpakato na Mgao wa kompyuta hizi umezingatia uwiano kati wanachuo na vifaa vilivyopo katika Vyuo vyetu kwa sasa,”amesema.
Vyuo vya Ualimu vilivyopatiwa Kompyuta ni pamoja na Marangu,Kleruu,Vikindu,Patandi,Korogwe,Mpwapwa,Shinyanga,Ilonga,Tarime,Tandala,Butimba,Mtwara na Morogoro.
Amesema dhima ya Vyuo vya Ualimu nchini ni kuandaa walimu mahiri na wanaotosheleza mahitaji katika shule za Awali, Msingi na Sekondari.
“Kutokana na dhima hiyo, Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji katika Vyuo vyote vya Ualimu vya Serikali nchini mkazo ukitolewa katika uboreshaji wa miundombinu, vifaa vya kujifunzia na kufundishia na matumizi ya TEHAMA kama nyenzo muhimu katika ufundishaji na ujifunzaji. Uboreshaji huu unakwenda sanjari na maendeleo makubwa katika matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika ufundishaji na Ujifunzaji,”Amesema.
Hata hivyo amesema Wizara inaendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika Vyuo mbalimbali nchini ikiwemo ukamilishaji wa Chuo cha Kabanga, Ujenzi wa vyuo vipya vya Sumbawanga, Dakawa, Mhonda na Ngorongoro unaendelea.
Aidha amesema kuwa ukarabati na ujenzi wa baadhi ya miundombinu katika vyuo vya Morogoro, Mpwapwa, Tukuyu, Kasulu, Butimba na Patandi nao unaendeleana huku ukitarajiwa kukamilika mwaka huu wa fedha 2021/2022.
““Hadi sasa Wizara imetoa mafunzo ya matumizi ya Tehama katika kufundishia na kujifunzia kwa wakufunzi wote 2,300 kutoka Vyuo vya Ualimu vya Serikali yote 35,”amesema.
“Hii itasaidia kupunguza uwiano wa matumizi ya kompyuta kwa Wanachuo kutoka Wanachuo 28 kwa Kompyuta moja hadi kufikia Wanachuo 2 kwa Kompyuta 1 vyuoni,”amesema.
Pia Prof.Mkenda amewaagiza wakuu wa vyuo hao kutunza Kompyuta hizo ambapo amesema Kompyuta hizo zimenunuliwa kwa gharama kubwa hivyo kila Mkuu wa Chuo kuhakikisha kuwa zinatumika kwa malengo ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji Chuoni.
“Kila Mkuu wa Chuo ahakikishe mali zote za Serikali zinatunzwa ipasavyo ili kuleta tija ya fedha zilizotumika na Vyuo vyote vya Ualimu vizingatie matumizi sahihi ya kompyuta hizi ikiwemo kuhaikikisha ziko katika mazingira yaliyo safi na salama kama ilivyo kanuni na taratibu za kutunza na kuhifadhi vitu vya TEHAMA,”amesema.
Awali,Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga amesema bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu nchini hivyo kunahitajika jitihada ili kuzaliwa walimu wengine wengi kupitia vyuo hivyo.
“Kila mwaka ni lazima tuzalishe walimu wa kutosha,Serikali ni kweli imewekeza ila bado kuna changamoto ya walimu bila walimu hatuwezi kutoka nyinyi ni chemchem ila tunaenda kubadilisha mitaala tutaangalia haya masuala ya teknolojia,”amesema.
Kwa upande wake,Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof. Caroline Nombo amesema mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Canada ambapo amedai mchango wa Canada katika mradi huo ni jumla ya Dola za Canada milioni 53.
Amesema mchango wa Serikali ya Tanzania ni katika kugharamia shughuli mbalimbali za uendeshaji wa vyuo ikiwemo gharama za malipo ya chakula kwa wanachuo na mafunzo ya ualimu kwa vitendo.
Prof.Nombo amesema dhumuni kuu la mradi huo ni kuendeleza elimu ya ualimu,kwa kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji kupitia uboreshaji wa miundombinu ya utoaji wa mafunzo ya ualimu katika vyuo vya ualimu vya Serikali 35.
“Utoaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.Kuimarisha mifumo na miundombinu ya tehama.Kuwaendeleza kitaaluma na kuwajengea uwezo watendaji katika utoaji wa elimu ya ualimu,”amesema.
Prof.Nombo amesema hadi kufikia Disemba mwaka 2021 jumla ya Dola za Canada milioni 42 sawa na asilimia 79.25 ya fedha zote za mkataba zilikuwa zimepokelewa kutoka kwa mfadhili wa mradi Globar Affars Canada.
Amesema hadi kufikia Disemba 2021 wastani wa utekelezaji wa malengo ya mradi ulikuwa ni asilimia 75.83.