Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt.Albina Chuwa,akifungua mafunzo ya kuwajengea uelewa walimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari pamoja na Maafisa Elimu Mkoa wa Dodoma kuhusu uhamasishaji kwa jamii katika ushiriki wa sensa ya watu na makazi yaliyofanyika jijini Dodoma.
Kamishna wa Sensa ya watu na Makazi Zanzibar,Balozi Mahammed Ally Hamza,akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa walimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari pamoja na Maafisa Elimu Mkoa wa Dodoma kuhusu uhamasishaji kwa jamii katika ushiriki wa sensa ya watu na makazi yaliyofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uelewa walimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari pamoja na Maafisa Elimu Mkoa wa Dodoma kuhusu uhamasishaji kwa jamii katika ushiriki wa sensa ya watu na makazi yaliyofanyika jijini Dodoma.
Afisa elimu mkoa wa Dodoma Gift Kyando,akielezea zaidi jinsi walivyojipanga kutoa elimu kwa jamii kuhusu Sensa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa walimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari pamoja na Maafisa Elimu Mkoa wa Dodoma kuhusu uhamasishaji kwa jamii katika ushiriki wa sensa ya watu na makazi yaliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa walimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari pamoja na Maafisa Elimu Mkoa wa Dodoma kuhusu uhamasishaji kwa jamii katika ushiriki wa sensa ya watu na makazi yaliyofanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………
Na.Alex Sonna,DODOMA
Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt.Albina Chuwa amesema asilimia kubwa ya nchi za Afrika zimeiga [ku-copy na ku-paste]mfumo wa sensa wa kushirikisha Zaidi walimu katika zoezi hilo.
Dkt.Chuwa ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa utoaji mafunzo ya kuwajengea uelewa walimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari pamoja na Maafisa Elimu Mkoa wa Dodoma katika uhamasishaji kwa jamii katika ushiriki wa sensa ya watu na makazi zoezi litakalofanyika Mwezi Agosti mwaka huu.
Dkt.Chuwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Masuala ya takwimu barani Afrika amesema nchi nyingi za Afrika zimeendelea kuiga na kupata uzoefu wa Tanzania katika kuendesha masuala ya sensa hasa kwa kutumia walimu wa msingi kuwa makalani na wasimamizi wa sensa.
“Mimi ni mwenyekiti wa Bara la Afrika Masuala ya Takwimu,kwa hiyo nchi nchi nyingi za Afrika zimeendelea ku-Copy na ku-paste kutoka Tanzania masuala ya uendeshaji zoezi la sensa kwa kuwatumia walimu ,zoezi letu la sensa tutaendelea kuwashirikisha ikiwemo kutoa mafunzo ,na safari hii hatutumii tena karatasi ,unamaliza mtu wa mwisho kuhesabu sisi tunajua idadi makao makuu muda huohuo”amesema.
Aidha,Dkt.Chuwa amesema kundi la walimu ni kundi muhimu katika kuhamasisha wanafunzi na jamii kwa ujumla katika ushiriki wa sense huku akizungumzia umuhimu wa sensa ni pamoja na kupata takwimu sahihi kwa ajili mipango ya taifa kuleta maendeleo.
“Ni mara ya kwanza kukutanisha kundi la walimu mkoa wa Dodoma na kuwaelezea umuhimu wa sensa,akina mama mnafahamu huwezi ukachota mchele ukapika kilo ishirini kama una watu wawili nyumbani ,hata mama zetu mama Ntilie ni lazima aangalie nini nikaweke wapi hii biashara yangu ,na yeye anahitaji takwimu hizi”amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema walimu ni mwanga muhimu kwa jamii hivyo kuna uhitaji mkubwa wa kuwajengea uwezo.
“Sisi kama mkoa tumeona walimu ni mwanga muhimu kwa jamii hivyo wakijengewa uwezo wakaelewa itasaidia sana katika uhamasishaji suala la sensa”amesema.
Aidha ameitaka ofisi ya Taifa ya Takwimu kufika katika halmashauri nyingine kutoa mafunzo ya umuhimu wa sensa ili kuyajengea uwezo makundi mbalimbali ikiwemo maafisa elimu,pamoja na walimu.
Naye Kamishna wa Sensa ya watu na Makazi Zanzibar,Balozi Mahammed Ally Hamza amesema ni wajibu muhumu kwa walimu kuwatumia wanafunzi kuwafundisha kuhusu sensa ili jamaii ikaelewa zaidi.
Ikumbukwe kuwa Tanzania hushiriki zoezi la sensa kila baada ya miaka 10 na sensa ya mwaka huu itakuwa ni sensa ya 6 na inatajwa ni kwa mara ya kwanza itafanyika kwa kidijitali na zoezi hili muhimu likitarajiwa kufanyika Mwezi Agosti na tarehe itapangwa na mamlaka husika.