Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt Francis Michael akizungumza na wadau wa Maliasili na Utali nchini, Dar es Salaam (hawapo pichani) Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Malikale Bw Donatius Kamamba akitoa shukrani kwa Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt Francis Michael (hawapo pichani) kwa niaba ya washiriki wa Mkutano wa miongozo ya uwekezaji katika maeneo ya Malikale nchini
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt Francis Michael akimsililiza mmoja wa wadau wa Utalii nchini, katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Malikale nchini Dkt Kristowaja Ntandu
Wadau wa Utalii nchini wakiendelea na majadiliano kuhusu miongozo ya uwekezaji katika maeneo ya Malikale nchini
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt Francis Michael (katikati mstari wa mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Utalii nchini.
***********************
Na Sixmund J. Begashe
Wizara ya Maliasili na Utalii nchini imeweka mkakati wa kuhakikisha maeneo ya Malikale nchini yanakuwa rafiki kwa wawekezaji ili kuvutia watalii zaidi, kuinua pato la taifa pamoja na kuwawezesha wanchi kiuchumi.
Hayo yamesemwa Jijini Ilala Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Francis Michael alipokuwa akifungua rasmi kikao cha wadau wa Utalii na wataalam wa Malikale ili kujadili miongozo ya uwekezaji katika maeneo ya Malikale nchini.
Licha ya kuwashukuru wadau hao kwa kuitikia wito na kuudhuria kikao hicho, Dkt Michael amesema majadiliano hayo yataleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya Utalii na kwa matumizi endelevu ya urithi wa Utamaduni kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.
“Malikale ni matokeo ya harakati za binadamu za kupambana na mazingira katika shughuli zake za kila siku. Kwa mantiki hiyo, malikale ni mali ya wadau wote. Aidha, ni urithi kutoka kizazi kilichopita, kinachoishi na kijacho. Hivyo, matumizi yake yanapaswa kuzingatia kizazi cha sasa na vijavyo”. Dkt Michael
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Malikale nchini Dkt Kristowaja Ntandu, ameleza kuwa japo utalii wa Malikale unazidi kukuwa kwa kasi, lakini wameona haja ya kukaa chini na wadau wa Utalii ili kupeana miongo ya namna bora ya uwekezaji katika maeneo hayo ili kazi ya uhifadhi iwe endelevu.
”Upo umihimu mkubwa wa uwekezaji katika maendeo ya maikale nchini ili kuvutia watalii zaidi, lakini tumeona ipo haja ya kuhakikisha usalama wa urithi huu ili kizazi kijacho nacho kije kufaidi, ndio maana tupo hapa na wadau ili kupeana miongozi na namna bora ya uhifadhi” Alisema Dkt Ntandu
Naye Afisa Mwandamizi wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw Gaudence Masi amesema hadi sasa uwekezaji umefanyika kwenye maeneo mengi zaidi ukilinganiasha na kwenye maeneo ya Malikale, hivyo ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kuwekeza kwenye maeneo hayo.
Bi Tetula Okama ambaye ni Mwongoza wageni licha ya kuipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuona umuhimu wa kukutana na wadau, anaishauri Serikali kutoa nafasi zaidi ya uwekezaji kwa wazawa kama sehemu ya kuwainua kiuchumi na kutengeneza ajira zaidi kwa wahitimu wa vyuo vikuu nchini.
Lengo la mkutano huo ni kuboresha miongozo ya uwekezaji katika malikale ili iweze kusaidia namna bora ya kutumia malikale sio kwa manufaa ya kiuchumi tu bali pia kijamii kama nyenzo ya kuliweka pamoja Taifa.