Mhe. Waziri Mchengerwa akitoa salamu za Serikali kwenye usiku wa Mahaba ndi ndi ndi
Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi akiwatambulisha mawaziri wanaosomamia Sanaa na Habari kwenye usiku wa Mahaba ndi ndi ndi Februari 14, 2022
Mtendaji Mkuu wa Wasafi na Msanii nguli Afrika Diamond Platinum akiongea kwenye Usiku wa Mahaba ndi ndi ndi Februari 14, 2022
Mwanamuziki Zuchu akitumbuiza katika Usiku wa Mahaba ndi ndi ndi Februari 14, 2022.
Wasanii mbalimbali wakitumbuiza
……………………………………………..
Na. John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameipongeza Kampuni ya Wasafi kwa kukuza sanaa ya muziki na kuzalisha ajira kwa vijana wengi hapa nchini.
Akizungumza kwenye hafla ya Usiku wa Mahaba Ndi Ndi Ndi siku ya wapendanao Februari 14, 2022 jijini Dar es Salaam amesema Wasafi ina mchango mkubwa katika kuibua na kukuza vipaji vya wanamuziki.
” Naomba nikuhakikishie Serikali ipo pamoja na nyie katika kukuza sanaa ” amesema Mhe.Mchengerwa
Aidha, amesema Serikali inakwenda kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wasafi mtaa kwa mtaa, kijiji kwa kijiji hadi mkoa kwa mkoa kutafuta vipaji vya wasanii lengo ni kuwashindanisha na kuwaendeleza.
Ameongeza kuwa, wizara inakwenda kuendeleza mapinduzi ya ukuzaji wa Sanaa ili kutoa ajira zaidi kwa vijana katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Amefafanua kwamba kufanya hivyo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya kutaka kuboresha sekta hiyo ili wasanii nchini waweze kunufaika na kazi zao.
Kwa upande mwingine Mhe. Mchengerwa amesema, katika kipindi hiki sanaa inakwenda kutumika kuitangaza Tanzania kimataifa.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wasafi, Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya barani Afrika, Diamond Platinum ameishukuru Serikali kwa kuendelea kujenga mazingira wezeshi kwenye Sekta ya Sanaa nchini.