Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akizungumza na watumishi ambapo amewataka kufanyakazi kwa ushirikiano na kufanya kazi kwa bidii katika kikao baina ya watumishi wa wizara, Taasisi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akizungumza na watumishi wa Wizara na Taasisi ambapo amesisitiza umoja, upendo na kufanya kazi kwa weledi katika kikao baina ya watumishi wa wizara, Taasisi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga.Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Prisca Lwangili akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri katika kikao baina ya watumishi wa wizara, Taasisi na Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Esther Kazenga akifanya utambulisho wa watumishi katika Idara mbalimbali na Taasisi zilizondani ya Wizara kwenye kikao baina ya watumishi wa wizara, Taasisi na Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Daniel Pancras (kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Aron Msigwa (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa TEHAMA, Mtani Yangwe (kulia) wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye Kikao kikao baina ya watumishi wa wizara, Taasisi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akizungumza wakati wa Kikao baina ya watumishi wa wizara na Taasisi zilizopo chini ya wizara kilichofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.Mkurugenzi Msaidi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Daniel Pancras (kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Aron Msigwa (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa TEHAMA, Mtani Yangwe (kulia) wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye Kikao kikao baina ya watumishi wa wizara, Taasisi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja kilichofanyika leo jijini Dodoma.
***********************
DODOMA.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja amewataka watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wawe mstari wa mbele katika kuhamasisha na kutangaza utalii ili kuvutia watalii wengi zaidi kwenda kutembelea vivutio vilivyopo hapa nchini.
Mhe. Mary ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo na Taasisi zake ambapo amesema kuwa iwapo kila mtumishi ataamua kutumia nafasi yake kutangaza utalii mwamko wa Watanzania kutembelea vivutio vilivyopo utaongezeka.
‘’Tunatakiwa sisi wenyewe tuoneshe mfano kwa kutafuta masoko na kuhamasisha Utalii, kutafuta mikutano mbalimbali inayo fanyika maeneo ije kufanyika Tanzania tuuze huduma za kumbi zetu za Kimataifa, bidhaa na bidhaa zetu kupitia hiyo mikutano” Amesema Mhe. Mary Masanja.
Amesema kuwa kupitia kuuza fursa hizo na mazao mbalimbali ya Utalii yaliyopo hapa nchini hususani mikutano ya Kimataifa itakuwa kichocheo kwa watalii wengi kuhamasika kufika kwenye vivutio vilivyopo.
Mhe. Mary Masanja amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila wizara na taasisi kutangaza utalii hatua itakayosaidia kuongeza Pato la Taifa kupitia watalii wanaokuja kutembelea vivutio hivyo hapa nchini.
Aidha, katika hatua nyingine Naibu Waziri Mhe. Mary Masanja ametoa wito kwa Wanawake wote wa Wizara hiyo kuyatumia Maadhimisho yajayo ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayoadhimishwa Machi 8 mwaka huu kupaza Sauti zao kwa kuhamasishana kutangaza Utalii wa ndani na kutembelea vivutio vilivyopo.
‘’Sasa hivi tumekuwa na matukio ya watu kujiua, tunataka tupunguze tatizo hili kwa kufurahi kukutana pamoja ,kubadilisha mawazo . Tunataka kuanzia tarehe 1 mpaka 8 mwezi Machi mwaka huu sisi wenyewe tuutangaze utalii wetu’’ Amesisitiza
Katika hatua nyingine, Mary amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu na upendo na kuepuka mambo yayonarudisha nyuma utendaji wao mahali pa kazi huku akiwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa ushirkiano ili Sekta ya Utalii izidi kusonga mbele.