………………………………………………….
Na Lucas Raphael,Tabora
Shirika la World Vision Tanzania limewezesha wananchi wapatao 5000 kunufaika na mradi mkubwa wa maji ya kisima katika wa kijiji cha wita kata ya ndala wilaya ya nzega mkoani Tabora utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 500 hadi kukamilika kwake.
Mradi huo wa maji ya kisima kirefu wanaotarajiwa kusambazwa katika Zahanati na shule ya msingi wita ambao unatarajiwa kumilika wiki mbili zijazo.
Akizunguza wakati akikagua mradi huo Katibu Tawala wa wilaya ya Nzega Onesmo Kisoka alisema wadau wa maendeleo kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia RUWASA waharakishe kukamilisha mradi huo ili wananchi waweze kupata maji.
Alisema wananchi wanaitaji kupata maji haraka kwani miundombinu yote imeshakamilika tatizo ni Ruwasa wanakwama wapi kwa ajili ya kusambaza mabomba kwa wananchi wa vitongoji vinane vya kijiji cha wita.
Hata hivyo aliwataka wahandisi wa Ruwasa kuhakikisha wanasambaza mabomba haraka na wananchi wanapata maji ili kuweza kumtua mama ndoo kichwani
“Kinamama wanatumia muda urefu na umbali mrefu wa kwenda kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kushindwa kufanya shughuli nyingine ya maendeleo ya familia yake kwa kuongeza kipato cha familia “alisema Kisoka
Naye Kaimu meneja wa Ruwasa wilaya ya Nzega Mhandisi Faustini Makoka alimweleza katibu Tawala huyo kwamba serikali imeshawapatia fedha kwa ajili ya kukamilisha miundombinu ya maji na kukamilisha usambazji wa mabomba kwa wananchi kwenye vitongoji vinane .
Alisema kwamba wananchi watapata maji hivi karibu kwani kila kitu kimekamilka ilikuwa bado Ruwasa kukamilisha matengenezo kidogo kwenye tanki .
Mhandisi Makoka alisema kwamba kisima hicho kinauwezo watoa maji mengi safi na salama na kuongeza pampu inauwezo wa kusukuma maji milimita za ujazo 15,000 kwa saa ambapo tanki linauwezo wa kuhifadhi maji milimita za ujazo 100,000.
Mratibu wa wa mpango wa maendeleo ya Jamii wa shirika la World Vision Tanzania, Michael Ngasa alisema katika mradi huo walishikiana na Ruwasa waligawana majukumu ilikuweza kufanikisha mradi kwa wananchi wa kijiji cha Wita.
Alisema kwamba mpango wa maendelea Ndala ulikuwa na kazi ya uchimbaji wa kisima katika eneo la (Bohehole),ujenzi wa nyumba ya Pampu ,Ununuzi na ufungaji wa Pampu na sola za umeme .
Vinginne vilivyofanyika ni ununuzi na ulazaji wa bomba toka kwenye chanzo cha maji hadi kwenye Tanki la kuhifadhi maji pamoja na ujenzi na usambazaji maji kwenye vijijji vinne vya kuchotea maji kwenye magati ya maji mitaani(DPs) ambapo kazi hiyo ilikamilika kwa ufanisi mkubwa .
Kijiji cha wita kata ya ndala wilaya ya nzega wananchi wake walikuwa wanafuata maji umbali mrefu lakini kupatikana kwa maji kijijini hapo adhaa kwa wanawake na watoto imepungua