Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Spora Liana akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo |
Sehemu ya madiwani wakifuatilia kikao hicho
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya
Jiji la Tanga limepitisha mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Jiji kwa mwaka
2022/2023 ya kiasi cha shillingi za Kitanzania Billion 73 ambazo zitatokana na
mapato ya vyanzo vya ndani, ruzuku na wahisani.
Bajeti hiyo imepitishwa katika Mkutano
wa Baraza la Madiwani uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano
wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza baada ya kupitishwa kwa
bajeti hiyo Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo alisema bajeti
hiyo imegusa maeneo yote muhimu kwa maendeleo ya Jiji hilo na wananchi wake
Alisema kwa upande wa mapato ya
vyanzo vya ndani, Halmashauri imekadiria kukusanya kiasi cha shillingi Billion
16, huku nguvu za wananchi katika uchangiaji wa miradi ya maendeleo
zikikadiriwa kuwa shillingi Million 824.6, huku fedha za kutoka Serikali kuu na
wahisani zikikadiriwa kuwa shillingi Billion 56.
Akizungumzia mpango wa maendeleo
katika mwaka wa 2022/2023 Halmashauri
imekasimia kutumia jumla ya shillingi Billion 19.9 kwa ajili ya miradi ya
maendeleo ambapo Billion 13.1 ni fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu na
wahisani na shillingi Billion 6.7 ni fedha za mapato ya ndani na nguvu za
wananchi na michango ya fedha taslim makadirio yakiwa ni million 824.
Alisema kwa upande wa miradi
halmashauri hiyo itatumia Billion 6.7 za mapato ya ndani kwa mwaka 2022/2023
katika utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.
Aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa
ni Mfuko wa utoaji mikopo ya wanawake, vijana na wenye ulemavu kiasi cha sh.
Billion 1.2, Ujenzi wa barabara za lami kupitia Tarura sh. Billion 1.2,
Ukarabati wa kituo cha Afya Pongwe, Ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule za
Msingi na Sekondari, Ukarabati wa masoko ya Makorola, Kisosora na Majengo,
Ujenzi wa nyumba za watumishi.
Alisema suala lingine ni Ukamilishaji
wa vyumba vya maabara katika shule za Sekondari,
Ujenzi soko la samaki Deep Sea,
Uwezeshaji wa kituo cha Tanga TV, Ujenzi wa shule mpya ya Msingi ya English
Medium, Kupima viwanja 500 kwenye maeneo ya Amboni, Tongoni, Mabokweni na Ndaoya.
Aidha aliitaja miradi mengineyo kuwa
ni Halmashauri hiyo imetenga fedha za uendeshaji wa ofisi za Kata na za Mitaa,
ambapo kiasi cha shillingi Million 20 kitatolewa kila baada ya miezi mitatu
katika kata zote 27, na kiasi cha shillingi 200,000.00 kimetengwa kutolewa kwa
kila mtaa kwa kila robo mwaka.
Wakizungumzia bajeti hiyo madiwani
wa Halmashauri hiyo kutoka kata mbalimbali Jijini Tanga walionekana kuridhishwa
nayo kutokana na kuakisi maendeleo ya wananchi.
Akizungumza bajeti hiyo Diwani Viti Maalumu
katika Jiji hilo (CCM) Mwanaidi Kombo
alisema bejeti hiyo imepita kwa furaha kwa sababu imeongezeka karibia Bilioni 1
na vile vipaumbele vya wananchi
vimeanishwa ikiwemo suala la vijana,walemavu na masuala ya miradi ya maendeleo
Alisema pia ikiwemo miradi ya kimkakati ambayo
imeingizwa kwenye bajeti hiyo na itakuwa chachu kwenye kuakisi
maendeleo,masoko,hospitali,vituo vya afya
vimeingizwa jamboa ambalo ni muhimu kwa ustawi wa maendeleo.
Naye kwa upande wake Diwani wa Kata ya Chongoleani (CCM) Mwaveso
Mbega alisema bajeti hiyo imekidhi vigezo vinavyotajika kwa ajili ya maendeleo
ya Jiji la Tanga kwa sababu imekusanya karibia vitu vyote vinavyohitaji kwenye
maendeleo ikiwemo elimu,afya ,miundombinu ya b arabara,vijana wakina mama na
walamevu.
Alisema ukiangalia bajeti ipo vizuri
na wanaamini kutokana na mipango yao madiwani kwenye kusimamia ukusanyaji wa mapato na serikali ni sikuvu yenye
kuwajali watu wake na wana matumaini mafungu nafasi inayoichangia kuweza bajeti
hiyo itakuja kwa ajili ya kukamilina na mambo yatakwenda vizuri.