*************
Azam Media Limited (AML) inautaarifu umma kuwa wafanyakazi wake 12 waliokuwa wanakwenda mkoani Mbeya kwa ajili ya kazi ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya NBC wamepata ajali baada ya gari lao kusukumwa na lori lililokuwa likirudi nyuma kwa dharura katika Mlima Kitonga, Iringa.
Ajali hiyo imetokea mchana wa leo Jumapili, Februari 13, 2022.
Kwa msaada mkubwa wa ofisi ya mkuu wa Mkoa, kikosi cha Polisi Mkoa wa Iringa na Mganga mkuu wa Mkoa, majeruhi wamechukuliwa na matabibu wa Mkoa wa Iringa kwa matibabu.
Uongozi wa Azam Media Limited unawashukuru wote waliotoa msaada wa hali na mali na kuwaomba Watanzania wote kuwaombea majeruhi nafuu ya mapema.
Imetolewa na
Azam Media Limited
13.Februari.2022