……………………………………………..
NJOMBE
Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Daniel Mwilango kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Nickson Myamba (48) aliyekuwa katibu wa baraza la walei katika kanisa la Roman Katoliki kigango cha Parokia ya Makambako yaliyotokea tarehe 8 February 2022.
Katika mauaji hayo yaliyotekelezwa katika duka la vitabu vya kiimani lililopo mkabala na kanisa inaelezwa yamehusisha mtumishi wa kanisa ambaye alikuwa ni katekista huku sababu ikitajwa ni chuki binafsi dhidi ya marehemu aliyekuwa katibu wa parokia.
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumtia nguvuni mtuhumiwa kamanda wa jeshi la polisi mkoani Njombe Hamis Issa amesema mtuhumiwa amekamatwa katika eneo la Doma lililopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambapo amekutwa akiwa na vitu mbali mbali vya marehemeu ikiwemo simu ya mkononi.
“Baada ya kutendeka kwa tukio jeshi lilianza upelelezi na jambo la kustaajibisha mtuhumiwa amekamatwa wilayani Mvomero Morogoro akiwa na simu ya marehemu,Alisema kamanda Issa”
Mara baada ya kuhojiwa Kamanda Issa anasema mtuhumiwa amekiri kuhusika na kisha kuonyesha vitu mbali alivyotumia kutekeleza mauaji likiwemo Panga aliliokuwa amelitupa katika choo,chuma , ndoo na vitambaa vilivyotumika kusafisha damu katika chumba yalipotendeka mauaji.
Katika hatua nyingine jeshi linamshikilia mlinzi wa kanisa hilo aliyetambulika kwa jina la Nickson Valentine kwamadai ya kwamba kuna mahusiano ovu na mtuhumiwa wakati tukio likitekelezwa.