**************
Na Joseph Kayinga
Zaidi ya Makocha 150 wa mpira wa miguu jijini Dsm leo wamefungua ukurasa mpya na kuukaribisha mwaka 2022 kwa kujumuika pamoja kupitia Bonanza la michezo katika uwanja wa Karume Jijini Dsm.
Jumuiko Hilo limewaleta pamoja walimu wa mpira wa miguu kutoka manispaa zote 5 za Jiji la Dsm ambalo linaunda mikoa mitano ya kisoka.
Kongamano hilo limeandaliwa na Chama Cha makocha wa mpira wa miguu nchini (TAFCA Taifa) Kwa pamoja na makatibu wa mikoa hiyo mitano ya kisoka ya Dsm.
Akiongea juu ya umuhimu wa kukutana, kufahamiana na kubadilisha uzoefu Kwa kuzingatia mabadiliko ya mpira wa miguu Duniani, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Bw. Oscar Mirambo ameeleza kufurahishwa na hatua Hiyo ya TAFCA kuandaa tukio hilo huku akiahidi kutoa Ushirikiano wa dhati kwa matukio mengine kama hayo yatakayoandaliwa siku zijazo.
Kabla ya nasaha za Mkurugenzi huyo WA Ufundi wa TFF, Katibu wa TAFCA Taifa Bw. Mohamed Tajdin, ameeleza kuwa bonanza hilo ni mwanzo tu, Huku akielezea kuwa litafuatiwa na matukio mengine mengi kama hayo baadaye.
Pamoja na hotuba za Viongozi hao, makocha kadhaa walioshiriki tukio hilo wameeleza kuwa itapendeza kama na matukio ya kuwakutanisha pamoja makocha yakafanyika mara kwa mara.
Wengine wamependekeza kuwa yasiishie Dar es salaam tu bali yahusishe makocha wa mikoa mbalimbali zaidi ya Dsm.