Meneja Miradi wa PESACO Bw.Abel Swai akitoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Al-haramain iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam, Elimu hiyo ni mwendelezo wa Kampeni ya Mkinge Mwanafunzi Dhidi ya Ajali za Barabarani. Mwenyekiti wa PESACO Bw.Mfaume Hassani akitoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Al-haramain iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam, Elimu hiyo ni mwendelezo wa Kampeni ya Mkinge Mwanafunzi Dhidi ya Ajali za Barabarani.
Katibu wa PASACO Bw.Fransisco Peter akitoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Al-haramain iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam, Elimu hiyo ni mwendelezo wa Kampeni ya Mkinge Mwanafunzi Dhidi ya Ajali za Barabarani. Wanafunzi wa shule ya Sekondari Al-haramain iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam, wakiwasikiliza wataalamu kutoka Taasisi ya PESACO wakitoa elimu ya Usalama barabarani ambapo ni mwendelezo wa Kampeni ya Mkinge Mwanafunzi Dhidi ya Ajali za Barabarani.
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na utoaji elimu ya Usalama barabarani (PESACO) limeendelea na kampeni yake ya “Mkinge Mwanafunzi Dhidi ya Ajali za Barabarani” kwa kutoa elimu ya usalama barabarani katika shule za Msingi na Sekondari nchini.
Akizungumza katika zoezi hilo lililofanyika katika shule ya Sekondari Al-haramain iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa PESACO Bw.Mfaume Hassani amesema ajali za barabarani zimezidi kua miongoni mwa vyanzo vikubwa vinavyo chukua uhai wa watu wengi na kusababisha majeraha na ulemavu kwa maelfu ya watu.
Amesema Umoja wa mataifa na shirika la afya duniani wanakadiria kuwa watu zaidi ya milioni 1.3 hupoteza maisha kila mwaka, idaidi hii ikiwa ni mara mbili ya vifo vinavyosababishwa na Malaria na UKIMWI. Vifo vingi na majeraha hutokea zaidi katika nchi za uchumi wa kati na zinazoendelea kama Tanzania.
“Ili kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani PESACO imejizatiti kuunga mkono jitihada za serikali na vyombo vyake katika kuhakikisha tunafikia Tanzania isio na ajali. Tukitumia nyenzo ya elimu PESACO inayafikia makundi yote sita ya watumia barabara, kuwapa elimu stahiki itakayowasaidia kudumisha uwiano wa matumizi salama ya barabara ili kuepukana na ajali”. Amesema Bw.Hassani.
Pamoja na hayo Bw.Hassani amesema zoezi hilo ni endelevu kwani mpaka sasa wameshawafikia wanafunzi zaidi ya elfu mbili (2,000) ambapo kwa hakika elimu walioitoa itasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa ajali za barabarani.