************************
Naibu Waziri wa Kilimo Mh Anthony Mavunde akizungumza na Menejimenti ya Bodi ya Mkonge Tanzania baada ya kukagua ukarabati wa jengo la ofisi la Bodi ya Mkonge Jijini Tanga.
Naibu Waziri Mavunde amewataka Menejimenti ya Bodi ya Mkonge kuleta matokeo chanya ya ukuaji wa uzalishaji wa zao la Mkonge kwa kuja na ubunifu utakaochochea kilimo hicho cha Mkonge na kuwasisitiza kutofanya kazi kwa mazoea na badala yake wahakikishe wanaacha alama katika tasnia ya Mkonge.
Naibu Waziri yupo Mkoani Tanga kwa ziara ya siku mbili ambapo pia atapata nafasi ya kutembelea Kiwanda cha kuchakata mkonge cha SISALANA ,Kituo cha Utafiti wa Kilimo MLINGANO na kutembelea mashamba ya Mkonge wilayani Korogwe.