Mkurugenzi wa Shirika la ADLG, Jimmy Luhende, akitoa mada kwa waandishi wa habari washiriki wa kongomano la Maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani lililoandaliwa na Shirika la INTERNEWS ikishirikiana na Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC) kupitia Mradi wa Boresha Habari.
Waandishi wa habari, watangazaji wa redio na waawakilishi wa vituo vy redio wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilisha kwenye kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani lililofanyika jijini Mwanza kimkoa.Picha zote na Baltazar Mashaka.
***********************
NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza
TEKNOLOJIA ya Habari na Mawasiliano nchini inakua kwa kasi huku Redio ikibaki kuwa chombo muhimu cha upanashanaji habari kinachoifikia jamii kwa haraka.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhandisi Robert Gabriel,jana akifungua kongamano la waandishi na wadau wa habari lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani humu (MPC) ikishirikiana na Shirika la Kimataifa la INTERNEWS ili kuongeza uelewa na mwamko wa jamii kuhusu maadhimisho ya siku ya redio duniani.
Alisema Dunia inapoadhimisha Siku ya Redio kutimiza miaka 111,Tanzania imekuwa ikikua kwa kasi katika Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari huku redio zkitoa taarifa haraka zikifuatiwa na magazeti pamoja na luninga.
Mhandisi Gabriel alisema vyombo vya habari ikiwemo redio vina jukumu kubwa la kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za ukweli na zinazowapa nafasi ya kufahamu uhalisia wa mambo kupitia redio na kueleza umuhimu wa waandishi wa habari kufuata maadili yao ya kazi ili kuilinda jamii dhidi ya migogoro isiyo ya lazima.
“Redio ni chombo muhimu chenye nguvu na kinachoaminiwa katika kuwafikia watu wengi kwa haraka na wakati mmoja,gharama nafuu na kupata taarifa kwa usawa,kinazungumza na mhusika moja kwa moja na kinajenga umoja wa jamii,”alisema Mhandisi Gabriel.
Alikumbusha wana habari mkoani Mwanza kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na kuepuka kuwa nje ya miiko ya taaluma ya habari,ili mkoa usikike kwa maendeleo ingawa wapo wachache wanapotoka kwa maslahi yao ambapo maudhui ya mwaka huu ni “Redio na Uaminifu”.
Alisistiza Siku ya Redio inapoadhimishwa leo Februari 13 mwaka huu,Tanzania itaendelea kuunga mkono vyombo hivyo na kwamba Shirika la Kimataifa la INTERNEWS kufanya kongamano la waandishi na wadau wa habari mkoani Mwanza ili kuongeza mwamko na uelewa wa siku hiyo kwa jamii ni jambo la kupongezwa.
Mratibu wa Shirika la
INTERNEWS Shaban Maganga,alisema wanatoa huduma kwenye nchi 100 duniani wakivijengea uwezo vyombo vya habari kwa kuvipa vifaa,ruzuku na mafunzo kwa waandishi wa habari ili kuwaongezea maarifa ya kufanya kazi kwa ubora,weledi na kuzingatia maadili.
Alisema siku ya redio ni muhimu kwa jamii na inapaswa kutambua kazi kubwa inayofanywa na chombo hicho hivyo mwamko unahitajika na kuipa kipaumbele siku hiyo kwa maslahi ya umma kutokana na tija iliyoongezeka kupitia redio.
“Kongamano hili ni Mradi wa Boresha Habari,tumeliandaa kwa ufadhili wa USAID lengo mahususi la kuifanya siku ya redio kuwa ya kipekee, kuboresha utendaji kazi, kuongeza ujuzi, maarifa na kukumbushana maadili,kuongeza mwamko na umuhimu wa kazi zinazofanywa na redio katika jamii ya pembezoni,”alisema Maganga.
Kongamano hilo kupitia mada mbalimbali kuliibuliwa changamoto zinazoikabili redio, zikiwemo sheria zisizo rafiki zinazosimamia sekta ya habari,maudhui na kukosekana sera ya uhariri kwenye redio nyingi nchini pamoja na mchango wa redio kwenye maendeleo nchini.
Aidha Rose Mwanga, katika mada yake ya nguvu ya redio katika uwajibikaji alisema redio imewezesha jamii kuibua na kuhoji masuala mbalimbali kwa maslahi yao na kuwafanya viongozi serikali, kisiasa na Asasi za Kiraia kuwajibika.
Ofisa Habari wa Jiji la Mwanza kwa niaba ya Ofisa Habari wa Mkoa,Remija Salvatory,alieleza namna serikali inavyofanya kazi na redio za jamii na imekuwa ikitumia chombo hicho kama kiunganishi kikubwa baina ya jamii na serikali kwa kuwa ni vigumu kuwafikia wananchi wengi kwa wakati mmoja.