……………………………………………………
Na.Mapuli Misalaba, Shinyanga
Waendesha Bodaboda na Bajaji katika manispaa ya Shinyanga wameziomba taasisi za kifedha kuona namna bora ya kutoa mikopo yenye masharti nafuu kuliko hivi sasa ambapo wamedai mikopo inayotolewa ina masharti magumu,ikilinganishwa na uwezo wa wahitaji.
Wametoa kauli hiyo leo wakati taasisi ya kurasimisha rasilimali na Biashara za wanyonge MKURABITA kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ilipotoa semina kwa makundi ya wafanyabiasharia wa kati wakiwemo waemnda Bodaboda na Bajaji.
Wamesema taasisi hizo zikiwemo Benki zimekuwa zikitoa mkopo wenye masharti magumu ambapo inawawia vigumu wafanyabiashara wa kati wakiwemo bodaboda na bajaji ambao kipato chao hakiwezi kukidhi matakwa ya mikopo hiyo.
kwa upande wake afisa mahusiano wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Venance Amani amesema atafikisha maombi hayo kwenye taasisisi hiyo ili kuona namna ya kuweza kuwasaidia wafanyabiashara wa kati.
Kwa upande wake Afisa maendeleo wa Manispaa ya Shinyanga Bestina Gunje amesema Halmashauri hiyo inatoa mikopo ya asilimia kumi kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu hivyo amewasisitiza vijana kuwa waaminifu hasa kwenye marejesho pale wanapopata mkopo.
Aidha akizungumza katika semina hiyo mtaalam wa sheria kutoka katika taasisi ya mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania bwana Harvey Kombe ametoa wito kwa wafanyabiashara kujitokeza kwenye semina kuwasikiliza watoa huduma ili kuimarisha biashara.
Semina hiyo imeandaliwa na taasisi ya mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA kwa kushirikiana na ofisi ya mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga ambapo itahihimishwa tarehe 16/2,2022.