WAZIRI wa Maji Mhe.Jumaa Aweso,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini ya mikataba 86 ya mradi ya miundombinu ya Maji.
WAZIRI wa Maji Mhe.Jumaa Aweso,akisisitiza jambo wakati wa hafla ya utiaji saini ya mikataba 86 ya mradi ya miundombinu ya Maji.
Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji pamoja na watendaji wa RUWASA wakati wa hafla ya utiaji saini ya mikataba 86 ya mradi ya miundombinu ya Maji.
MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Almas Maige,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini ya mikataba 86 ya mradi ya miundombinu ya Maji.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mhandisi Clement Kivegalo,akitoa taarifa wakati wa hafla ya utiaji saini ya mikataba 86 ya mradi ya miundombinu ya Maji.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Dodoma Dk. Godfrey Mbabaye,akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso (hayupo pichani) wakati wa hafla ya utiaji saini ya mikataba 86 ya mradi ya miundombinu ya Maji.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mhandisi Clement Kivegalo (kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Lukolo Ltd Bw.Burton Msemwa wakisaini makubaliano wakati wa hafla ya utiaji saini ya mikataba 86 ya mradi ya miundombinu ya Maji
……………………………………………………….
Na.Alex Sonna,DODOMA
WAZIRA ya Maji kupitia Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), umesaini mikataba 86 ya ujenzi wa miundombinu ya Maji yenye thamani ya Sh.Bilioni 309.99
Akishuhudia utiaji saini leo jijini Dodoma Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
amekemea wakandarasi watakaofanya ubabaishaji kwenye miradi hiyo huku akiwataka watendaji wa Mfuko wa maji kuweka taratibu nzuri za malipo ya wakandarasi.
“Mfuko wa Maji wekeni mfumo mzuri na nitaufumua na kuweka utaratibu mzuri ili mtu akiwasilisha hati ya malipo apewe fedha aende kufanya kazi,”amesema.
Hata hivyo, ametaka kuwapo na ushirikishwaji wa wananchi na wabunge katika kutekeleza miradi hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa RUWASA, Mhandisi Clement Kivegalo amesema kuwa RUWASA imepanga kutekeleza miradi 1,527 ambapo kati ya miradi hiyo miradi 351 ilikuwa ya utafutaji wa vyanzo vya maji na usanifu wakati miradi 1,176 ni miradi ya ujenzi wa miundombinu
Mhandisi Kivegalo amesema kuwa Sehemu ya miradi 1,176 ni miradi ambayo imeibuka mwaka wa fedha uliopita ambayo ni 317 huku miradi mipya ni 462 wakati miradi ya ukarabati na upanuzi ilikuwa 397.
”Hali ya utekelezaji wa miradi hiyo, miradi 317 iliyovuka mwaka, miradi 249 imekamilika na inatoa huduma ya maji wakati miradi ile 397 ya ukarabati na upanuzi ambayo inatekelezwa kwa mfumo huku miradi 301 ikikamilika na kutoa huduma ya maji”amesema Mhandisi Kivegalo
Alifafanua katika miradi iliyopita 462, miradi 138 ilitangazwa makao makuu ya RUWASA ili kupata wakandarasi na miradi 324 ilitangazwa na mameneja wa mikoa 25 kwa kutumia bodi za uzabuni