***********************
Na John Walter-Babati
Msanii maarufu wa Hiphop nchini Tanzania P-Mawenge amesema ngoma mpya ya My Future Wife ni ngoma ambayo inamhusu kila mtu kwa namna alivyoandika Mashairi ya wimbo huo.
Wimbo wa P. Mawenge ni kama filamu kwa namna alivyoandika kiustadi akizungumzia mahusiano kwa mtu ambaye alitoa moyo wake wote kumpenda mpenzi wake ila baadaye akatendwa.
Akizungumza na Smile Fm redio kwenye kipindi cha Power Point na Isiaka Mc amesema katika ngoma zake zote”My Future wife” ni ngoma nyingine kali anayoielewa wakati wote.
Katika ngoma hiyo P Mawenge anasema “Ulipotoka kwenu ni mimi ndo ulinifuata,ingawa mabwana zako mjini walishajipata,ila kwa sababu tu kijijini walikukacha,ukaona bora tu utulie na mimi tuanze chapter,nikakupa mahaba na ukadata nayo sana,nikajua lile penzi tungezikwa nalo mama”
Amewaomba Mashabiki waendelee kusapoti kazi zake ambazo zinapatikana you tube kwenye akaunti ya P-Mawenge na mitandao mingine yote ya kijamii.
Video ya My Future wife imetayarishwa na Director Kezzy wa Kurunzi Studio na audio imetengenezwa na Producer Franken katika studio za Bantu Music Dar es salaam.