………………………………………………..
MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameihoji serikali ni lini itatenga fedha kwa ajili ya kununua meli ya mazoezi katika Chuo Cha Bandari (DMI),kilichopo Jijini Dar es salaam.
Akiuliza swali la nyongeza Februari 10 bungeni,Mtaturu amesema Chuo hicho kilichopo Ukanda wa Afrika Mashariki ni muhimu sana kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo.
“Kwa sababu vijana wanaoenda kufundishwa pale wanatakiwa kufundishwa kwa vitendo na chuo hiki kina tatizo la kuwa na meli ya mazoezi ,Je ni lini serikali itatenga fedha kwa ajili ya kununua meli ya mazoezi?,”alihoji.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na Ajira Patrobas Katambi amesema serikali imeshatenga fedha kwa ajili ya kufanya maboresho mbalimbali.
“Nimuhakikishie Mh Mbunge katika suala hilo kuwa zipo fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya vifaa vya kufundishia na kwenye hili suala la meli ni sehemu ya mpango huo,na kadri upatikanaji wa fedha utakavyokuwa watakamilisha hilo,”alisema.