Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga,akipanda mti katika eneo la Tambukareli Dodoma leo Februari 11,2022, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa kesho Februari 12,2022 jijini Dodoma na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Edward Nyamanga,akipanda mti katika eneo la Tambukareli Dodoma leo Februari 11,2022, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa kesho Februari 12,2022 jijini Dodoma na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
Balozi wa Mazingira na Mbunge wa Pandani, Mariam Omary Saidi,akipanda mti katika eneo la Tambukareli Dodoma leo Februari 11,2022, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa kesho Februari 12,2022 jijini Dodoma na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Dk. Andrew Komba,akipanda mti katika eneo la Tambukareli Dodoma leo Februari 11,2022, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa kesho Februari 12,2022 jijini Dodoma na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
Mkurugenzi wa huduma ya kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Beatrice Mutayoba ,akipanda mti katika eneo la Tambukareli Dodoma leo Februari 11,2022, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa kesho Februari 12,2022 jijini Dodoma na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
Meneja wa BOT Tawi la Dodoma Dkt. Wilfred Mbowe,akipanda mti katika eneo la Tambukareli Dodoma leo Februari 11,2022, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa kesho Februari 12,2022 jijini Dodoma na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
Wadau mbalimbali wakipanda miti katika eneo la Tambukareli Dodoma leo Februari 11,2022, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa kesho Februari 12,2022 jijini Dodoma na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga,akizungumza na wanafunzi na wananchi walioshiriki zoezi la kupanda miti katika eneo la Tambukareli Dodoma leo Februari 11,2022, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa kesho Februari 12,2022 jijini Dodoma na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
Balozi wa Mazingira na Mbunge wa Pandani, Mariam Omary Saidi,akizungumza na wanafunzi na wananchi walioshiriki zoezi la kupanda miti katika eneo la Tambukareli Dodoma leo Februari 11,2022, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa kesho Februari 12,2022 jijini Dodoma na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Kanda ya Kati, Mathew Kiondo,akizungumza na wanafunzi na wananchi walioshiriki zoezi la kupanda miti katika eneo la Tambukareli Dodoma leo Februari 11,2022, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa kesho Februari 12,2022 jijini Dodoma na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
…………………………………………………….
Na.Alex Sonna,DODOMA
MAKAMU wa Rais, Dk.Philip Mpango anatarajiwa kuzindua Sera mpya ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 utakaofanyika kesho Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Hayo yamesemwa leo Februari 11,2022 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga,wakati akiwaongoza wanafunzi na wananchi walioshiriki zoezi la kupanda miti katika eneo la Tambukareli Dodoma, ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa kesho.
Bi.Maganga amesema kuwa katika wiki hii wananchi wamehamasika na kujitokeza kufanya shughuli mbalimbali zilizopangwa ikiwamo kupanda miti na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.
“Kila tulipokwenda kwa ajili ya kupanda miti tunakuta umati mkubwa wa watu, mwamko ni mkubwa na watanzania wamehamasika na kesho ni kilele cha shughuli hii yote tunahitimisha kwa kuzindua sera mpya ya mazingira,”amesema Bi.Maganga
Kwa upande wake Naye, Balozi wa Mazingira na Mbunge wa Pandani, Mariam Omary Saidi,amewataka wakazi wa Dodoma kuhakikisha wanaitunza miti na mazingira ili kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.
Awali, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Kanda ya Kati, Mathew Kiondo,ametaka miti hiyo kutunzwa baada ya msimu wa mvua kuisha na kudhibiti mifugo.
“Si vizuri tukapanda miti leo halafu mwakani tena tunapanda sehemu hii hii tutakuwa tunapoteza nguvu na fedha za serikali kwa hiyo tuhakikishe tumepanda leo, tuite mkutano kama huu kuja kumwagilia maji kwa kuwa Dodoma kipindi cha ukame ni kirefu,”amesisitiza