katibu wa
MACHINGA mkoa wa Iringa Joseph akiongea na wafanyabiashara wagodo wadogo manispaa ya Iringa wakijdali mstakabali wao wa kuhama maeneo ya mashine tatu na miomboni
katibu
wa
MACHINGA mkoa wa Iringa Joseph akiongea na wafanyabiashara wagodo wadogo
manispaa ya Iringa wakijdali mstakabali wao wa kuhama maeneo ya mashine
tatu na miomboni
Na Fredy Mgunda,Iringa
Uongozi wa umoja wa
wafanyabisahara wadogo wadogo (MACHINGA) Manispaa ya Iringa wamesema kuwa anaekwamisha
zoezi la wao kupangwa vizuri ni meya wa manispaa ya Iringa na sio kiongozi
mwingine na kusababisha mgomo wa kwenda eneo la welfare kufanyia shughuli zao
za kibiashara.
Akizungunza na blog hii katibu wa
MACHINGA mkoa wa Iringa Joseph Kilienyi alisema kuwa wamekuwa wakifanya
majadiliano mara kwa mara na viongozi mbalimbali wa wilaya na mkoa wa Iringa
juu ya swala la MACHINGA kuhamia katika eneo la Makabuli ya Mlandege lakini
kikwazo kimekuwa kwa meya wa manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa wamewapangia eneo
ambalo sio rafiki kwa biashara ambazo wanazifanya hivyo wameamua kugoma
kuondoka katika maeneo ambayo wanafanyia biashara hivi sasa.
Kilienyi alisema kuwa serikali ya
manispaa ya Iringa imewapangia wahamie katika eneo la welfare ambalo wanadai ni
dogo halafu sio Rafiki kwa baishara ambazo wanafanya kwa kuwa ni vigumu wateje
kuwafikia katika eneo hilo.
Alisema kuwa hayo yote yanakuja
kwa shirinikizo la Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada ambapo wahajui
anamaslai gani na maeneo hayo yote mawili ambayo anataka machinga waende
kufanyia biashara zao.
Kilienyi alisema kuwa waliushauri
uongozi wa wilaya,mkoa na manispaa ya Iringa kuwa eneo ambalo ni Rafiki kwa ajili
ya biashara za MCHINGA ni pembezoni mwa makaburi ya Mlandege ambako kuna
mzunguko mkubwa wa wananchi na kwao itakuwa rahisi kufanya biashara zao.
Aliongeza kuwa mara baada ya
kuona swala hilo limekuwa gumu kwao walipeleka hoja binafsi kwenye baraza la
madiwani ili madiwani waweze kuijadili kwa kina swala hilo lakini Meya wa
Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada aliitupilia mbali hoja jambo ambalo wanadai
lilizua maswali mengi vikwani mwao.
Kilienyi alisema kuwa uongozi wa
manispaa ya Iringa ulishauriwa kuweka uzio kuyazunguka makaburi hayo na sehemu
ya nje ya uzio ndio yatakuwa Rafiki kwao kufanyia biashara tofauti na maeneo ambayo
wanapangiwa bila kushirikishwa na kiongozi huyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa MACHINGA
mkoa wa Iringa Yahaya Mpelembwa alisema kuwa haoni hoja ambayo imekuwa
ikimpelekea meya Ngwada kulikataa ombi la wafanyabiashara hao kwenye kufanyia
biashara zao pembezono mwa makaburi ya Mlandege.
Mpelembwa alisema kuwa uongozi wa
mkoa Iringa chini ya mkuu wa mkoa wa Queen Sendiga na mkuu wa wilaya ya Iringa
Mohamed Moyo ulikubari ombi lao lakini meya amekuwa kikwazo kwa kulikataa ombi
hilo.
Naye aliyekuwa mwenyekiti wa
MACHINGA mkoa wa Iringa Zeche Zabron alisema kuwa wafanyabisha hao wanatakiwa
kwenda katika makaburi ya Mlandege tu na sio sehemu nyingine kwa kuwa makaburi
hayo yanaweza kuondolewa kwa kuwa yamekaa miaka mingi ambayo kisheria
yanatakiwa kuondolewa kwa kufuatatu utaratibu husika.
Alisema hakuna sheria
inayokatakaza makaburi kuhamishwa hivyo ameutaka uongozi wa manispaa ya Iringa
kuhakikisha wanayaoondoa makaburi hayo kwa mujibu wa sheria za nchi kama
ambavyo inatakiwa la sio watalazimika kwenye mahakani kwa hoja ya kuyaondoa
makaburi hayo.
Zeche alisema kuwa tatizo pale kuna
kaburi la babu yake meya wa Iringa Ibrahim Ngwada ndio maana imekuwa tatizo
kwake lakini makaburi yale tayari yameshapitwa na muda hivyo yanatakiwa
kuondolewa au kuwekea uzio ili MACHINGA wahamie kufanya biashara zao pale.
Alisema kuwa wafanyabiashara
wadogo wadogo (MACHINGA) mkoani Iringa wataendelea kuugomea uongozi wa manispaa
ya Iringa kuhama katika eneo la mashine tatu na miomboni ambalo wanafanyia
biashara zao hivi sasa hadi pale watakapo ambiwa wahamie Mlandege.
Akijibia kero hizo Meya wa
manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alisema kuwa kila hatua wanayoifanya ya
kuwahamisha MACHINGA katika manispaa hiyo wamekuwa wakiwashirikisha viongozi
wao mara kwa mara anashangaa kuona wameanza kuyageuka majadiliano yao.
Alisema kuwa walikubaliana na
viongo wa umoja huo kuwa eneo Rafiki kwa biashara yao ni eneo la welfare na
serikali ikawekeza fedha nyingi ambazo zimetumika kujenga mabanda ya kufanyia
biashara na yamekamika sasa anashangaa kuona kumeanza maneno mengine ambayo
hayana afya kwa maendeleo ya manispaa ya Iringa.
Ngwada alisema kuwa viongozi wa
MACHINGA wamekuwa wakilitaka eneo la makaburi ya Mlandenge jambo ambalo ni gumu
kufanyika kutokana na historia ya makaburi hayo.
Ngwada alisema kuwa ili kuyaondoa
makaburi hayo ni lazima kuwashirkisha wananchi,viongozi wa dini wizara husika
na kutathimini gharama halisi ya makaburi hayo na kuingalia sheria inasema na
vyote hivyo havijafanyika na viongozi wa MACHINGA Iringa wanataka tu yaondoke
wapewe eneo hilo wafanyie biashara.
Alisema kuwa kuhusu hoja yao
kupeleka kwenye baraza la madiwani haikufuata wala haikuzingatia sheria na
kanuni za baraza la madiwani wa manispaa ya Iringa ndio maana hoja hiyo
haikusomwa mbele ya madiwani na wananchi wengine waliohudhuria baraza hilo.
Alisema kuwa watu waliozikwa
katika eneo hilo wanathimini kwa mchango wa kimaendeleo walioufanya hadi
kuifikisha manispaa ya Iringa ilipofika hivyo sio japo jepesi kiasi hicho cha
kuyaondoa makabuli hayo.
Ngwada alisema kuwa kuna maeneo
mengi ambayo MACHINGA wa Manispaa ya Iringa wanatakiwa kufanyia biashara sio
eneo ambalo holo wanalolihitaji kwa kutumia mashinikizo bila kujali wataalam
wanasema nini.