WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mita(TAMISEMI),Innocent Bashungwa,akipokelewa na Kaimu rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Mwalimu, Dina Mathamani mara baada ya kufika katika hafla ya Utoaji wa Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa Mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara iliyofanyika leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mita(TAMISEMI),Innocent Bashungwa,akisalimiana na katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzanaia (CWT ),Mwalimu, Deus Seif,mara baada ya kufika katika hafla ya Utoaji wa Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa Mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara iliyofanyika leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mita(TAMISEMI),Innocent Bashungwa,akizungumza wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa Mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara iliyofanyika leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.
KAIMU rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Mwalimu, Dina Mathamani ,akizungumza wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa Mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara iliyofanyika leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzanaia (CWT ),Mwalimu, Deus Seif,akisoma risala ,wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa Mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara iliyofanyika leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi , David Silinde,akizungumza ,wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa Mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara iliyofanyika leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki,akizungumza wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa Mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara iliyofanyika leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato,akizungumza wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa Mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara iliyofanyika leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akitoa salamu za Mkoa wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa Mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara iliyofanyika leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.
Sehemu ya walimu pamoja na wanafunzi wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa Mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara iliyofanyika leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mita(TAMISEMI),Innocent Bashungwa,akiwakabidhi tuzo walimu pamoja na wanafunzi wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa Mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara iliyofanyika leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mita(TAMISEMI),Innocent Bashungwa,akiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa Mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara iliyofanyika leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mita(TAMISEMI),Innocent Bashungwa amewataka wakuu wa shule zote nchini kusimamia miradi yote kwa ufasaha ili iendane na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali
Hayo ameyasema leo Februari 11,2022 jijini Dodoma kwenye hafla ya Utoaji wa Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa Mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara.
Amesema ili kufikia malengo ya serikali ni lazima kusimamia miradi yote kwa ufasaha na iendane na thamani ya fedha, na mali za shule zitunzwe kwa ufasaha ili ziweze kutumika na vizazi vijavyo.
“Natoa maagizo kwa wakuu wote wa shule nchini kuhakikisha kwamba wanasimamia sheria, miongozo na taratibu katika sekta ya elimu, kusimamia miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao, pamoja na kutunza majengo ili yatumike hata katika vizazi vijavyo,”amesema Bashungwa.
“Wapo baadhi yenu hawana mahusiano mazuri na jamii hivyo hukwamisha utekeleaji wa baadhi ya shughuli za serikali hasa miradi mnapokuwa na mahusiano mazuri na viongozi katika jamii hii pia inarahisisha katika utekelezaji na hata utunzaji wa majengo ya serikali,”amesema Bashungwa.
Kwa upande wake Kaimu rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Mwalimu, Dina Mathamani amesema wao kama walimu wameona umuhimu wa kutoa tuzo na pongezi kwa walimu waliofanya vizuri na kuwafanikisha wanafunzi kufaulu vizuri.
“ufaulu unaendelea kupanda siku hadi siku taaluma zinapanda na mazingira ya walimu yataendelea kuboreshwa na niahidi kwa niaba ya Chama cha walimu tutafanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha ufaulu unaongezeka ili tupate wataalamu katika sekta mbalimbali”amesema Mwl.Mathamani.
Awali katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzanaia (CWT ),Mwalimu, Deus Seif,amesema Chama kinatambua jitihada kubwa zinazofanywa na serikali katika kuboresha maisha ya watanzania wakiwemo walimu.
Aidha Mwl Seifa ameiomba serikali kulipa madai mbalimbali ya walimu ambayo bado yapo kwenye Halmashauri ili kuongeza ari ya kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi.
“Pia kuna madai mbalimbali ya walimu bado yapo katika Halmashauri zetu na hata Wizarani, likizo, matibabu, uhamisho, malimbikizo ya mishahara, madaraja, masomo tunaomba uhakiki wa mara kwa mara ufanyike na walimu walipwe ili kuongeza ari ya kufanya kazi,”amesema
Hata hivyo ameiomba Serikali kujengea nyumba za walimu hasa wa maeneo ya pembezoni ambapo kuna shida zaidi ya nyumba hata za kupanga.