Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwasilisha taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Ofisi kwa kipindi cha nusu ya mwaka 2021/22 na taasisi zake, kuanzia julai hadi Desemba.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy Nderianaga akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. John Jingu akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
Matukio katika picha wakati wa Jumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipokuwa wakipokea taarifa ya utekelezaji ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu)
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Kizito Mhagama akisisitiza jambo wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya waziri Mkuu kwa kipindi cha nusu ya Mwaka 2021/22.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Yahaya Masare akisisitiza jambo wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya waziri Mkuu kwa kipindi cha nusu ya Mwaka 2021/22.
…………………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Balozi Dkt. PIndi Chana amesema maagizo mawili ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria yalioyotolewa wakati wa kujadili makadirio ya bajeti ya Serikali ya Mwaka wa fedha 2021/22 ya Ofisi ya Waziri Mkuu yametekelezwa kikamilifu.
Balozi Chana amezungumza hayo wakati uwasilishaji wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu 9/February/2022 kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi kwa kipindi cha nusu mwaka 2021/22 na taasisi zake kuanzia Julai hadi Desemba 2021. Ofisi ya Waziri Mkuu imefanya vikao vya mashauriano na Wizara ya Fedha na Mipango ili kuhakikisha bajeti ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2022/23 inaongezwa na kutekelezwa kwa kuzingatia mahitaji halisi kama ilivyoelekezwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria. Maombi rasmi yametolewa kwa ajili ya kuzingatiwa wakati wa kutoa viwango vya ukomo wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Aidha Serikali imehakisha fedha zote zilizoidhinishwa na Bunge kwa ajili ya kuwezesha Ofisi ya Waziri Mkuu kutekeleza majukumu ya Uratibu, zinatolewa kwa wakati kwa lengo la kuwezesha Ofisi kutekeleza majukumu yake. Serikali imeendelea kuiwezesha Ofisi kwa kuipatia fedha zilizotengwa kwenye bajeti kila mwezi hadi Desemba 2021 mafungu manne ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Fungu 25 Ofisi Binafsi ya Waziri Mkuu, Fungu 37 Ofisi ya Waziri Mkuu, Fungu 27 Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Fungu 61 Ofisi ya Tume ya Uchaguzi kwa pamoja yamepokea T.sh Billion 3785,6357,683.88. sawa na 56% ya bajeti ya fedha ya T. sh. Billion 67331770000 iliyoidhinishwa kwa mafungu hayo amesema Balozi Dkt. Chana.
Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Katiba ya Bunge ya katiba na Sheria Katibu Mkuu anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amesema ujenzi wa ukuta wa Ofisi ya Waziri Mkuu upo katika hatua ya kuweka mfumo wa umeme na kuweka taa na kuimarisha ukuta, kukaa vizuri na kazi bado inaendelea.
Aidha kazi ya ujenzi wa kiwanda kipya na kufunga mita mpya ya Ofisi ya Mpiga chapa wa serikali iko mbioni kuanza, Mkandarasi ameshapatikana na maombi ya fedha yameshafanyika hazina baada ya muda mfupi matokeo yataonekana amesema Dkt. Jingu.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya bunge ya katiba na sheria Dkt. Joseph Kizito Mhagama imeipongeza Ofisi ya waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) kwa kusimamia na kutekeleza maelekezo ya kamati vizuri.