Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Angeline Mabula kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 09 Februari, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 09 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Ardhi Mhe. Angeline Mabula na Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kumuapisha Waziri Mabula katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 09 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluh Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson katika picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula mara baada ya kumuapisha katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 09 Februari, 2022.
.…………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amemuapisha Mhe. Dkt. Angeline Sylvester Lubala Mabula kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Mhe. Dkt. Mabula ameapishwa leo baada ya kuwa na udhuru wakati mawaziri wengine walipoapishwa mwezi uliopita.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Katika hatua nyingine, Rais Samia anatarajia kuondoka nchini kuelekea Ufaransa na baadae Ubelgiji kwa ajili ya ziara ya kikazi katika nchi hizo.
Akiwa nchini Ufaransa, Rais Samia anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani.
Rais Samia pia atashuhudia utiaji Saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa katika sekta za miradi ya maendeleo, ushirikiano katika masuala ya uchumi wa buluu, usalama wa bahari, sekta ya usafiri na maendeleo endelevu.
Pamoja na masuala mengine, Rais Samia pia anatarajiwa kuzungumza na Watanzania waishio nchini Ufaransa.