Waumini wa kanisa katoriki Parokia ya Makambako mkoani Njombe wamejikuta katika kiiza kinene na sintofahamu baada ya usiku wa februari 7 kukuta mwili wa Nickson Muyamba aliyekuwa katibu wa baraza la walei kigango cha Makambako ndani ya duka la vitabu vya kiimani akiwa amekatwa na kitu chenye ncha kali na kisha kutenganishwa mwili wake vipande viwili.
Katika misa ya mazishi iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu bikira Maria mama wa neema parokia ya Makambako Padre Jordan Mwajombe ambaye ni DEKANUSI wa Makambako amesema mauaji hayo ya kikatili ,hayaja fanywa kwa mpango wa mungu na kwamba yamelitia doa kanisa katorini kwa kutendeka katika eneo la kanisa na kwamba kanisa linakwenda kutenga siku 9 kwa ajili ya kufanya maombi maalumu ya marehemu na kuwafichua wahusika.
Serikali nayo imeshiriki misa na mazishi ya mtumishi huyo wa kanisa ambaye amepewa nafasi ya upendeleo ya kuzikwa katika viunga vya kanisa kwakuwa ameuwawa akiwa kanisani akiendelea na majukumu yake ,Ambapo mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa kwaniaba ya mkuu wa mkoa akalaani vikali mauaji hayo na kisha kueleza hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa kubaini wahusika wa mauaji ili kuwafikisha mahakamani.
Licha mauaji hayo kutekelezwa usiku wa kuamkia februari 8 lakini hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusika .