WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk. Damas Ndumbaro,akipokelewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga,mara baada ya kuwasili katika eneo la Iyumbu kwa ajili ya kupanda miti leo Februari 9,2022 , ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk. Damas Ndumbaro,akipanda Mti katika eneo la Iyumbu Dodoma leo Februari 9,2022, ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga,,akipanda Mti katika eneo la Iyumbu Dodoma leo Februari 9,2022, ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Dk. Andrew Komba,akipanda Mti katika eneo la Iyumbu Dodoma leo Februari 9,2022, ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Kamishna wa Hifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo,akimwangilia maji mti mara baada ya kupanda katika eneo la Iyumbu Dodoma leo Februari 9,2022, ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga,akiteta jambo na Kamishna wa Hifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo mara baada ya kupanda miti katika eneo la Iyumbu Dodoma leo Februari 9,2022, ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk. Damas Ndumbaro,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupanda Miti katika eneo la Iyumbu Dodoma leo Februari 9,2022, ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Dk. Andrew Komba,akielezea mikakati ya utunzaji mazingira mara baada ya kupanda Miti katika eneo la Iyumbu Dodoma leo Februari 9,2022, ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Kamishna wa Hifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo,akizungumza mara baada ya kupanda Miti katika eneo la Iyumbu Dodoma leo Februari 9,2022, ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk. Damas Ndumbaro,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Iyumbu Dodoma leo Februari 9,2022, ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk. Damas Ndumbaro,akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Iyumbu Dodoma leo Februari 9,2022, ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk. Damas Ndumbaro,akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya jiji la Dodoma walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Iyumbu Dodoma leo Februari 9,2022, ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
…………………………………………………..
Na.Alex Sonna,DODOMA
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk.Damas Ndumbaro,amewahimiza wananchi kutambua umuhimu wa kupanda miti katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha lengo ikiwa ni Kurejesha hali ya asili ya mazingira iliyoharibika kutokana na shughuli za kibinadamu na kuongeza kuwa upandaji miti ni kuweka mazingira safi.
Hayo ameyasema leo Februari 9,2022 wakati akiwaongoza wanafunzi na wananchi walioshiriki zoezi la kupanda miti katika eneo la Iyumbu Dodoma, ikiwa ni wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Dkt. Ndumbaro amesema kuwa lazima watanzania watumie njia hizo ili kuhakikisha maeneo yote yanakuwa yakijani nakuwataka wanafunzi ambao hawajapanda mti watekeleze zoezi hilo
Amewataka kuhakikisha Dodoma inakuwa ya kijana kwa kushirikiana na ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira pamoja na Maliasili na utalii kwani wao ni pacha na huwezi kutenganisha mazingira na misitu ikiwa kazi ya misitu ni kuweka mazingira sawa.
”Miti ni muhimu kwani bila nyuki hakuna kilimo,mkulima ategemea miti ili kuleta mvua na hali ya hewa nzuri ikiwa pia mfugaji anategemea msitu na bila msitu mifugo itakuwa pia binadamu tunategemea misitu katika shughuli zetu za kila siku.”amesema Ndumbaro
Dk.Ndumbaro amesema kuwa tukipanda miti lazima tupande miti ili kuifanya Tanzania kuwa ya kijani, kuna faida nyingi za misitu, kuna watu wanaishi kwa ajili ya kupanda misitu na hata nchi zingine misitu inachangia kiwango kikubwa sana kwenye GDP.
‘’Misitu inafanya kazi kubwa mbili kwanza inachukua hewa ya ukaa inaibadilisha na kutengeneza oxsgen kwani ndio hewa tunayoivuta sisi endapo tutakata miti yote hatutaweza kupata hewa safi maana yake tutakufa,ukiona mtu anakata miti ovyo ovyo ujue mtu huyo anatutengenezea kifo,’’amesisitiza Dk.Ndumbaro
Hata hivyo amebainisha kuwa kwa Tanzania asilimia 3.5 ya GDP inazidi sekta nyingine kutokana na umuhimu wa misitu.
Dkt.Ndumbaro amesema kuwa asilimia 54 ya eneo la Tanzania ni misitu zaidi ya hekta 400,000 ni misitu na inatunzwa kupitia TFS na wananchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mary Maganga ametoa wito kwa wananchi kuendelea kupanda miti kwenye makazi.
Bi. Maganga amesema zoezi la upandaji ni kielelezo cha kutoa hamasa na kuhamasisha maeneo mengine nchi nzima kupata uelewa kuhusu dhana nzima ya kuifanya nchi nzima kuwa ya kijani nay a mfano kupitia kampeni ya Kijanisha Dodoma.
Naye, Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Dk. Andrew Komba, amesema miongoni mwa mambo yaliyopo kwenye sera hiyo mpya ni masuala ya utunzaji wa rasilimali za misitu.
Dk.Komba amesema kutokana na jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na wadau mbalimbali ambapo imeendelea kuhifadhi maeneo ya misitu na asilimia 62 ya maeneo nchini yamehifadhiwa.