Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo Kiliani Myenzi akiwa sambamba na mwenyekiti wa wazazi pamoja na katibu wa vijana katika eneo la jenzi wa ofisi ya chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo ambapo wamepania kujenga ofisi ya kisasa kuliko ofisi zote wilaya za chama hicho Tanzania nzima
Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Kilolo NNA MPONELA MSOLLA akiwa anafanya usafi katika jengo linalojengw kuwa ofisi ya wilaya ya kilolo.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Chama cha mapinduzi Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa kimeipongeza
Serikali ya awamu ya sita kwa kufanikisha miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo
ya Maji uboreshwaji wa miundombinu ya barabara, Afya na elimu.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo Kiliani Myenzi alisema
Serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza kwa vitendo ahadi za
maendeleo kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani na kuchochea
maendeleo.
Kiliani Myenzi ameyasema hayo wakati wa hafla ya maadhimisho ya
miaka 45 ya CCM wilayani humo na kuwahimiza wananchi kuendelea kuunga mkono
jitihada za Serikali katika kuboresha maisha ya watanzania kupitia miradi ya
maendeleo.
Alisema kwa kipindi kifupi ambacho Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameingia madarakani amefanikiwa
kuboresha kila sekta kwa ajili ya kukuza uchumi wa wananchi na kuiletea
maendeleo wanananchi.
Myenzi
alisema kuwa wananchi wa wilaya ya kilolo mkoani Iringa wanamuunga mkono Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi
anazozifanya na wapo tayari kumpigania tena mwaka 2025 kwenye uchaguzi mkuu.
Aliesma kwa upande wa wilaya ya Kilolo amepeleka fedha nyingi
kutatua kero ya ya Maji uboreshwaji wa miundombinu ya barabara, Afya na elimu
na sasa wananchi wanafura na uongozi wake.
Nao baadhi ya wananchama wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kilolo
walisema kuwa wanaunga mkono kinachofanywa na mwenyekiti wa chama hicho ambaye
pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
kwa kazi kubwa anayoifanya ya keleta maendeleo kwa watanzania.