Mkuu wa Idara ya mazingira jiji la Dodoma Dickson kimaro,akizungumza na wanafunzi na wananchi walioshiriki kufanya usafi wa kufyeka kandokando mwa barabara, usafi wa mitaro na kuokota mifuko ya plastiki katika eneo la Nzuguni, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Idara ya mazingira jiji la Dodoma Dickson kimaro,akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanafunzi na wananchi walioshiriki kufanya usafi wa kufyeka kandokando mwa barabara, usafi wa mitaro na kuokota mifuko ya plastiki katika eneo la Nzuguni ,ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Nzuguni C Idrisa Bale ,akizungumza na wanafunzi na wananchi walioshiriki kufanya usafi wa kufyeka kandokando mwa barabara, usafi wa mitaro na kuokota mifuko ya plastiki katika eneo la Nzuguni, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Wananchi pamoja na wanafunzi wakifanya usafi wa kufyeka kandokando mwa barabara, usafi wa mitaro na kuokota mifuko ya plastiki katika eneo la Nzuguni ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Idara ya mazingira jiji la Dodoma Dickson kimaro akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki zoezi la kufanya usafi wa kufyeka kandokando mwa barabara, usafi wa mitaro na kuokota mifuko ya plastiki katika eneo la Nzuguni, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,DODOMA
WAKAZI wa jiji la Dodoma wametakiwa kuhakikisha wanafanya usafi kwenye maeneo yao yanayowazunguka kwa lengo la kulifanya jiji hilo kuwa na mazingira salama na yenye kuvutia.
Hayo yamesemwa leo Februari 8,2022 jijini Dodoma na Mkuu wa Idara ya mazingira jiji la Dodoma Dickson kimaro,wakati wa zoezi la kufanya usafi wa kufyeka kandokando mwa barabara, usafi wa mitaro na kuokota mifuko ya plastiki katika eneo la Nzuguni, ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Kimaro amesema kuwa usafi wa mazingira katika jiji la Dodoma imekuwa ni ajenda ya kila siku katika kuhakikisha mazingira yanaendana na jina la makao makuu ya nchi.
”Suala la usafi ni la tabia ambalo linatakiwa kuanza na wananchi wenyewe kipande kichofanyiwa usafi kinaonena kuwa na muonekano mzuri Dodoma ni Makao makuu ya nchi sula hilo la usafi ni chachu kila mmoja ahakikishe mita tano kutoka nyumba yake hadi kwa jirani yake kumefanyiwa usafi”amesema Kimaro
Amesema kuwa kwa wafanyabiashara za mighawa, hoteli,nyumba za kulala wageni wametakiwa kufanya usafi kwa sababu usafi ni ustaarabu na una anza na mtu mwenyewe.
Zaidi ya asilimia 75 hadi 80 ya magonjwa yanayowakupata wananchi yanatokana na uchafu hiyo usafi unapofanyika ni njia mojawapo ya kujinginga na magonjwa mablimbli.
Aidha Kimaro amewataka wananchi wenye maeneo ambayo hawajayaendelezwa kuyaendeleza na kuyafanyia usafi na kama wakishindwa wawaachie watu wenye uwezo la sivyo utaratibu wa kisheria utafuata wa kunyang’anywa viwanja hivyo.
Amesema kuwa Mkurugenzi wa jiji tayari alishatoa maelekezo ya maeneo hayo mmiliki akishindwa utaratibu wa sheria utafuata kutokana na kushindwa kuendeleza.
‘Kuna baadhi ya watu wamepewa viwanja kwa muda mrefu na wameshindwa kuviendeleza,maelekezo waliyopewa katika hati zao za viwanja hivyo yanaelekeza baada ya miaka mitatu wawe wameayaendeleza”amefafanua
“Nawashukuru sana wananchi wa Kata ya Nzuguni kwa kufanya usafi katika barabara hii ya kutoka Martin Luther na kuelekea kule Ilazo na kufika Wajenzi na usafi huu tutaendelea nao.Pia nawashukuru wanafunzi wote waliojitokeza kufyeka nyasi na kufanya usafi,”amesema Kimaro.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Nzuguni C Idris Bale, ameushukuru uongozi wa jiji hasa Idara ya Mazingira kwa ushirikiano wao na kuwaaahidi kuendelea kufanya usafi katika maeneo yao yaliyowazunguka.
“Tunaahidi kwa hali hii la kufanya usafi wa mazingira na sisi tutaendelea na utaratibu huu na hata mkija kurudi tena hamtakuta hali ya awali, pia nashukuru waandishi wa habari kwa kuwa tumekuwa wote tangu saa kumi na mbili asubuhi na kuweza kuhabarisha umma katika masuala ya usafi,”anasema.