*********************
Na Lucas Raphael,Tabora
Halmashauriya wilaya ya Nzega mkoani Tabora limepitisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya shiingili Bilioni 42.659,477,542 kwa mwaka wa fedha wa mwaka 2022 – 2023.
Akisoma mapendekezo ya mpango na bajeti hiyo mkurugenzi mtendaji wa halmashauriya wilaya ya Nzega, Kiomoni Kibamba alisema katika mpango wa bajeti ya fedha wanategemea kupata kutoka vyanzo vya ndani, ruzuku, kutoka serikali kuu na wadau wa maendeleo kutoka kwenye vyanzo vya ndani ya halmashauri ya Nzega.
Alisema kuwa Katika mapato ya ndani watengemea kupata kiasi cha shilingi bilioni 2.4 ambapo shilingi bilioni 1.5 ni matumizi ya kawaida na kiasi cha shilingi bilioni 15.6 ni fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Kiomoni alisema kwamba katika mwaka huu wa fedha wanatengemea ubora wa huduma za afya katika vituo vya afya na zahanati zake ambapo wamekusudia kununua dawa na vifaa tiba ili kuwepo na uhakika wa dawa katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya.
Alisema kuwa kuwajengea uwezo watoa huduma vituoni na ngazi za jamii juu ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Mkurugenzi huyo akizungumzia swala ya elimu ya msingi kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika kata za
Mwangoye,Ndala,Isagenhe,Mwamala,Ugembe ,Mambali ,Kamhalanga,Magengati,Muhugi,Tongi na Nkiniziwa.
Alizitaja kata zingine ni Isanzu,Milamboitobo,Mbutu,Mogwa,Mwantundu,Ikindwa,Utwigu na Semembela.
Aidha Mkurugenzi huyo wa halmashauri ya Nzega alisema idara ya elimu ya sekondari imepanga kutekeleza shughuli za kusimamia upanuzi wa shule 31 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.
Alisema kwamba halmashauri hiyo itasimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa shule 14 za sekondari Puge,Mwanhala,Nkiniziwa,Magengati,Mongwa,Ally,Muhungi,Mambali,Mizibaziba,Mabonde,Mbutu,Kalitu,Bukene na Mwamala.