Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Buriani akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa mafundi umeme na Tanesco kuhusu kanuni za ufungaji umeme za mwaka 2019.
Kaimu meneja wa Mamlaka ya Uthibiti wa huduma za Nishati na maji Ewura kanda ya kati Mhandisi Martin Maurus akifungua mafunzo kwa mafundi umeme na Tanesco kuhusu kanuni za ufungaji umeme za mwaka 2019 iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa huduma za Nishati na maji Ewura
MAFUNDI umeme wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Tabora katika kutona kuhusu kanuni za ufungaji umeme za mwaka 2019 iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa huduma za Nishati na maji Ewura.
Wakandarasi wa umeme wa Rea wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Tabora aanyonekana kwenye shati jeupi ni Imani Matubula
……………………………………………………….
Na Lucas Raphael,Tabora
Mafundi umeme Mkoani Tabora Wametakiwa kuchangamkia fursa za miradi ya kimkakati ambayo itafungua milango ya kazi ikiwemo mradi wa SGR na bomba la mafuta linalopita kilometa 149 katika eneo la Tabora.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Buriani alipokuwa akifungua mafunzo kwa mafundi umeme na Tanesco kuhusu kanuni za ufungaji umeme za mwaka 2019 iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa huduma za Nishati na maji Ewura iliyofanyika jana katika ukumbi wa Veta mkoani hapa
Alisema kwamba miradi hiyo mikubwa inatekelezwa kupitia mkoani hapa kuelekea mikoa ya Kigoma ,Shinyaga na Mwanza itawavutia wawekezaji na watu wa kawaida kuja kujenga nyumba na miradi ambayo itakayoitaji huduma ya mafundi umeme .
Alisema kwamba mafunzo hayo yatawaongezea uelewa wa kufahamu kanuni za uunganishaji mifumo ya umeme zinazowaongoza katika utekelezaji wa majukumu ya mafundi umeme kwa kufanya kazi na kuzingatia sheria za nchi.
Aidha Balozi Dkt Batilda Buriani aliwahimiza mafundi umeme kusajiliwa ili waweze kutambulika kisheria kwa kupatiwa Leseni ya kufanya kazi nchini.
“ikumbukwe kuwa umeme unatumika katika makazi ya wananchi ,Taasisi za serikali ,Ofisi za Serikali na katika maeneo ya shughuli mbalilmbali za kiuchumi,hivyo usalama wa mifumo ya umeme ni muhimu sana ili kuepuka madhara yanayotokana na uungaji wa mifumo ya umeme”alisema Balozi Dkt Batilda Buriani.
Hata hivyo Kaimu meneja wa Mamlaka ya Uthibiti wa huduma za Nishati na maji Ewura kanda ya kati Mhandisi Martin Maurus alisema kwamba kunamafundi wengi wasiosajiliwa na wanafanyakazi bila usimamizi (vishoka) na kazi zao nyingi zinafanyika chini ya kiwango na kutokea ajali ya moto .
Alisema kwamba vifaa wanavyovitumia havikidhi viwango na husababaisha ajali za moto ambapo fundi anayetumika asiye na elimu na ujuzi stahiki ndio chanzo cha nyumba nyingi kukumbwa na majanga ya aina hiyo.
Mhandisi Martin Maurus aliwasisitiza mafundi hao kuwa na lezeni ili kuweza kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi mkubwa na wenye tija kwa jamii .
naye mkndarasa anayetekeleza umeme wa vijijini Rea Imani Matubula alisema kwamba mafunzo hayo yatafungua rursa kubwa kwa mafundi mkoani Tabora na wilaya zake ambazo zinatengea umeme pia
Alisema kwamba umeme ndio Gunguzo kubwa na kiungo muhimu katika kukuza uchumi kwa wananchi na jamii inatuzunguka