Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akipanda miti katika eneo la wazi Medeli jijini Dodoma leo Februari 7,2022 kuelekea wiki ya uzinduzi wa Sera ya Tsifa ya Mazingira ya mwaka 2021 itakayozinduliwa Februari 12,2022 Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Februari 12, 2022.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga,akipanda miti katika eneo la wazi Medeli jijini Dodoma leo Februari 7,2022 ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Februari 12, 2022.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Abdallah Hamis Mitawi,akipanda miti katika eneo la wazi Medeli jijini Dodoma leo Februari 7,2022 ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Februari 12, 2022.
Wanafunzi mbalimbali na watumishi wa Serikali na Taasisi wakipanda miti katika eneo la wazi Medeli jijini Dodoma leo Februari 7,2022 ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Februari 12, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na wanafunzi kutoka shule mbalimbali na wananchi walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Medeli jijini Dodoma leo Februari 7, 2022, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Februari 12, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akisisitiza wakati akizungumza na wanafunzi kutoka shule mbalimbali na wananchi walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Medeli jijini Dodoma leo Februari 7, 2022,ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Februari 12, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupanda miti katika eneo la wazi Medeli jijini Dodoma leo Februari 7,2022 kuelekea wiki ya uzinduzi wa Sera ya Tsifa ya Mazingira ya mwaka 2021 itakayozinduliwa Februari 12,2022 Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Februari 12, 2022.
…………………………………………………
Na.Alex Sonna,DODOMA
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selamani Jafo amewataka Watanzania kupanda miti katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha lengo ikiwa ni Kurejesha hali ya asili ya mazingira iliyoharibika kutokana na shughuli za kibinadamu na kuongeza kuwa upandaji miti ni kuweka mazingira safi.
Waziri Jafo ameyasema hayo leo Februari 7,2022 Jijini Dodoma wakati akipanda miti eneo la Makulu Akishirikiana na wadau wa mazingira pamoja na wanafunzi kutoka shule mbalimbali ambapo amesema wanafunzi na jamii zote waweke utaratibu wa kupanda miti ili kutunza mazingira.
Dk.Jafo amesema kuwa lazima watanzania watumie njia hizo ili kuhakikisha maeneo yote yanakuwa yakijani nakuwataka wanafunzi ambao hawajapanda mti watekeleze zoezi hilo.
”Jenda ya mazingira ndiyo ajenda inayosababisha uchumi kuwa imara huku akiwataka wanafunzi kupeleka ujumbe kwa wazazi wao kushiriki katika zoezi zima la kupanda Miti katika maeneo yao.”amesema Jafo
Serikali imekuwa na mikakati mbalimbali katika kuhakikisha inatunza mazingira ili kuwa na mazingira safi miongooni mwa mikakati hiyo ni upandaji miti katika taasisi za serikali na binafsi nchini.
“Niziombe familia tumesema tuna lile jukumu la kupanda miti ili kuitendea haki Tanzania yetu, tufanyie kazi ajenda ya mazingira sababu maji yalipungua kwenye vyanzo vingi vya mabwawa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi,”amesema.
Shughuli nyingine zitakazotekelezwa katika wiki hiyo ni upandaji wa miti katika eneo la Iyumbu, Isern, maeneo ya barabara inayoanzia Chimwaga na Chuo Kikuu cha Dodoma kuelekea barabara ya Dodoma Dar es Salaam.
Aidha, usafi utafanyika pembezoni mwa barabara inayoanzia Shule ya Martine Luther hadi wajenzi kupitia Nzughuni, Ilazo, Ipagala na Area C, kutoa elimu kuhusu utenganishaji wa taka, kufanya usafi katika soko la Chang’ombe na utoaji wa elimu ya mazingira kwa wananchi na wadau kupitia vyombo vya habari.