……………………………….
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amemteua Msanii wa Muziki Mrisho Mpoto kuwa balozi wa Sekta ya Maji na atakuwa akiitangaza Sekta ya Maji kupitia kazi yake ya Sanaa anayoifanya, katika shughuli mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya msanii huyo nguli hapa nchini kuimba wimbo wenye maudhui bora na kusheheni takwimu sahihi kuhusu Sekta ya Maji katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa maji wa Bunda, mkoani Mara. Hafla hiyo imeongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Msanii Mrisho Mpoto ni mmoja kati ya wasanii bora wa muziki katika ukanda wa Afrika Mashariki, aliyebobea katika kutumia vionjo vya kiasili kufikisha ujumbe kwa hadhira.