MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akisisitiza jambo wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk. Fatuma Mganga,akielezea mikakati ya mkoa huo katika suala la elimu wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri,akielezea mikakati ya wilaya yake katika kutoa elimu pamoja na ufaulu wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda,akizungumzia ufaulu wa wilaya yake na mikakati yake wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa wilaya ya Chamwino Gift Msuya,akielezea mikakati ya ufaulu wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dk.Khamis Mkanachi ,akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
MKUU wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remedius Emmanuel,akielezea jinsi walivyojipanga katika wilaya yake kuongeza ufaulu zaidi wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru,akielezea jinsi anatakavyo wasaidia wanafunzi waliofanya vizuri kwenda kutembelea na kuongea na wanafunzi wengine katika shule mbalimbali wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Nishati na Maji (EWURA) Mhandisi Godfrey Chibulunje,akielezea wanavyosaidia suala la elimu katika mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Dodoma Dk. Godfrey Mbabaye,akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe,akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Viongozi mbalimbali na walimu wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya wanafunzi wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,(hayupo pichani) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya wakuu wa wilaya wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,(hayupo pichani) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka, akimkabidhi cheti Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mpwapwa Hildagarda Remy kutambua jitihada na umahiri wake katika ufundishaji wa somo la lake na kuwezesha wanafunzi zaidi ya kumi kufaulu kwa daraja ”A” katika mtihani wao wa kidato cha nne 2021 (CSEE) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka, akimkabidhi cheti pamoja na Madaftari Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato,Anthia Kachelenesa kwa kufanya vizuri katika mtihani wa Kidato cha nne (CSEE) 2021 na kupata ufaulu wa Draja la Kwanza kwa Tarakimu 1 (Single digit) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
……………………………………..
Na.Alex Sonna,DODOMA
SERIKALI ya Mkoa wa Dodoma imesema itawasomesha jumla ya wanafunzi 43 kutoka shule saba za Serikali waliofaulu mtihani wa kidato cha nne Mwaka jana na kupata ufaulu wa daraja la kwanza wa alama saba kwa Wavulana na wasichana alama saba hadi tisa kwa masomo ya kidato cha tano na sita.
Wanafunzi 43 waliohitimu kidato cha nne na kufaulu kwa daraja la kwanza alama 7 kwa wavulana na alama 7 hadi 9 kwa wasichana watasomeshwa kidato cha tano na sita toka shule za Godegode Mtera dam,Mlowa Barabarani,Lukundo,Dodoma Sekondari,Msalato girls na Mpwapwa Sekondari.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa Walimu na Wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya Mtihani wa kidato Cha nne na darasa la saba Mwaka 2021,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Antony Mtaka amesema kuwa watagharamia ada kwa wanafunzi hao pamoja na kuwanunulia vifaa vya shule yakiwemo madaftari lengo likiwa kuongeza motisha kwa wanafunzi na wazazi ili waendelee kufanya vizuri katika masomo yao.
Mtaka amesema kipaumbele chake ni elimu hivyo atahakikisha anapambana kwa kushirikiana na walimu kuongeza ufaulu wa Mkoa huo katika mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne.
” Kazi ya serikali ya Mkoa wa Dodoma kwa wanafunzi hawa ni kuwezesha na kuhakikisha ada na vifaa vinapatokana, wajibu wa mzazi utabaki katika suala la sare za shule, mzazi mtoto wako akipangiwa shule njoo na barua yake tuletee sisi tunampatia vifaa na pamoja na kulipa ada.Na leo tunawapatia madaftari 9 kila mmoja, “amesema.
Pia Mtaka amenunua alama “A” kwa shilingi 5000 kwa walimu waliowasaidia wanafunzi kupata alama hiyo huku akidai kwa mwaka 2022 atanunua kwa shhilingi 10,000 lengo likiwa ni kuzidi kuongeza motisha kwa walimu.
Aidha,Mtaka amemuagiza Afisa Elimu kuwandikia barua wakuu wa shule ili ziende kwenye matangazo ya bodi za Vijiji siku ya kufunnga shule wazazi waende kwenye kikao Cha shule lengo kuhakikisha wanafunzi wanafaulu.
Pia walimu wametakiwa kuwa wabunifu katika ufundishaji wao ikiwemo kuwasidia wanafunzi waweze kufaulu mitihani yao huku akifurahishwa na ubunifu ulioonyeshwa na baadhi ya walimu akiwemo Mwalimu wa Shule ya Sekondari Godegode ambaye alionyesha ubunifu katika ufundishaji wa masomo ya sayansi licha ya kutokuwa na vifaa vya kufanyia mazoezi kwa vitendo.
Vilevile,amezitaka Kamati za kitaaluma zikae na kuona namna yakuwa na mitihani ya mara kwa mara ili kupata namna nzuri ya maandalizi ya mitihani ya Sekondari hasa kwa kutembelea shule ya Sekondari Bunge kwani inawafunzi wanaotoka katika shule bora.
“Ufauru wa mtoto ni faida kwa Taifa hivyo maandalizi yanaanza na mzazi mwenyewe hivyo mzazi ana wajibu kuchangia,ikifika mahala wazazi wakaonanumuhimu wa elimu wataweza kusaidia Taifa,”amesema.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk.Fatma Mganga amesema kuwa tuzo hizo zitatoa hamasa kwa Walimu na Wanafunzi katika ufundishaji na kuwataka wadau mbalimbali kujitokeza katika kuwekeza kwenye suala la elimu.